Ramadhani Mponjika a.k.a MC Rhymson (shoto) na Joseph Mbilinyia a.k.a 2 Proud ama Mr II ama Mr Sugu wakipenana tano mjini bagamoyo jana walipohudhuria warsha ya siku tatu ya wadau wa muziki kuzungumzia tasnia ya muziki na matatizo ikiwa ni pamoja na wizi wa hakimiliki na hakishiriki. MC Rhyson ni mwanachama mwanzilishi wa kwanza unit, kundi la kwanza la bongoflava kuimba kwa kiswahili na hatimaye kuufanya muziki huo ukubalike. Mr II yeye ni muasisi wa marapa mmoja mmoja ambapo alipanda chati kwa nyimbo zake kibao ikiwa ni pamoja na bongo darisalaam. hivi sasa wote ni wanaharakati wa kumkomboa mwanamuziki wa bongo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Hapo Michuzi safi sana, nina picha zawadi kwako nitaibandika muda si mwingi kwangu. Huyu ni Thugu, wanamuita thugu mzee wa Moto Chini babake huyu sela noma sana maana ameweza kujenga himaya sana kimuziki. Safi sana Sugu Michuzi tupe hizo picha na za wasela wengine wanaotoa itikadi kama wale wa Tanga na yule sijui Mbando ambaye sasa ana kaseti iitwayo Alibamu.

    ReplyDelete
  2. Kwa kusimama kwao kidete kutetea wenzao japo wapo "wako safi" kimuziki ni ishara tosha kuwa bongo flava inapasua miamba na inakwenda mbali.My congratulations and thanks to both of them.Sijamuona Ras Nganyagwa tu hapo!

    ReplyDelete
  3. Mungu awabariki sana kwa kuendeleza safari ambayo inaendelea kuwa mkombozi wa vijana wengi sasa hivi! mark

    ReplyDelete
  4. kaka Michuzi shukrani sana kwa picha hiyo ya wakongwe wa RAP..RAA na SUGU...maanake hawa jamaa sijawaona tokea 1998/99..
    mike muhagama..i'still remember your RADIO ONE freestyle sessions
    ..yu played a big part too,to Uplift the Bongo-Flava movement..
    matunda tunayaona sasa..

    ReplyDelete
  5. Michuzi,
    Ahsante kwa picha.Nimefurahi pia kuona majina kama ya KBC na Mike Mhagama wakiweka maoni yao kwenye uwanja huu wa blogu.Mchanganyiko huu ni mzuri na ndio unaifanya roadmap yetu kuwa sawia zaidi.

    ReplyDelete
  6. Jeff mtazame kabisa KBC pale kwangu. Nadhani siku si nyingi atakuja naye huku tulizungumza sana Mheshimiwa. Vipi Mike Muhagama huu wapi tunakumis sana mbona nawe hufungui Gazeti Tando lako ili tupate busara na historia ya uzoefu wako huko pia?

    ReplyDelete
  7. Jeff,KBC na Mheshimiwa sana Makene.Nashukuru kuona michango yenu pia kwa ukarimu.Un'gamuzi wenu wa yaliyopita na shukurani vyanifanya nitake kurudi nyumbani kesho.Ninachoweza kunena kwa leo ni tuombe uzima,nyumbani ni nyumbani tu.

    ReplyDelete
  8. Mike I mean fungua blogu na wewe. Unayo mengi ya kuandika na kuhifadhi hasa historia za muziki. Hatuna mtu anayeblogu habari za muziki na sasa nadhani tukikupata wewe tutakuwa na nafasi ya kujiliwaza huko, maisha ya ughaibuni na hata nyumbani Bongo yanahitaji kujiliwaza kiasi fulani. Tunakungoja kama tunavyomngoja KBC. Nadhani nitampigia simu KBC jioni ya leo tujadili zaidi na ikiwezekana Mike waweza nipata hapa 956 292 1168

    ReplyDelete
  9. Michuzi pia tuanomba uendelee kutupatia pic za wasanii wa muziki mbalimbali ambao wameonyesha harakati za kweli katika kuukomboa muziki wa kitanzani na hata kufikia hapa tulipo, big up to mr 11, Rhymson na wengineo kibao

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...