bob rudala wa inafrika band akichangia katika warsha ya muziki bagamoyo leo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 17 mpaka sasa

  1. Michuzi hapa umenikumbusha 'kurefu'(kwa wengine samahani wanyaki hatunatofauti kati ya 'umbali' na 'urefu'). Unanikumbusha wimbo wa "Juli" na "Nimekuchagua wewe". Hasa huo wa kwanza. Si shaka mmeaza kuwaza kuwa nilipigwa-ga chini, partly you are right. But when in Bongo I will continue where I left. This time with some new tricks I learned from a chagga budy.

    Cha mno sikukumbuka-ga kubeba CDs za Bob Ludala.

    PS:'cha mno' ni lahaja ya Morogoro.

    ReplyDelete
  2. Nadhani awamu ya JK inatoa fursa nzuri sana ya watu kujadili ni wapi tulikosea...juzi walikuwa wadau ya kambumbu leo wadau wa muziki....nadhani tutafika....

    nashukuru kwa picha ujumbe...

    ReplyDelete
  3. wewe ndugu unaetumia sana hizo ga kwenye maneno yako zinabore,
    hivi huwezi tu kuandika kawaida mpaka uweke hizo ga?

    ReplyDelete
  4. Ndicho Kiswahili nilichojifunza-ga nikiwa-ga mdogo. Kiswahili changu kimeathiriwa-ga na Kinyakyusa. Pole kwa kuboreka.

    ReplyDelete
  5. we unacheka tu, na kunadika pumba tu, hivi ni kwanini unacheka? tena unanyakusudi kuandika utumbo mara zote? kcc

    ReplyDelete
  6. Ndio nilivyofundishwa-ga bwana kcc. Ukiiona pumba wengine pumba hiyo wanalisha wanyama wao then life goes on. Ntakushangaa kama wewe unataka kula pumba. We ukiona huwezi kuila iache, kakojoe kisha kalale.

    ReplyDelete
  7. Heshima tulifundishwa na tumeitumia kwa miaka mingi. Kama wapenda nawe heshima huna haja ya kuficha sura yako tukutazame. Thomas Jefferson aliwahi kunukuliwa akiwaambia wafanyakazi wa umma kuwa nanukuu na tafsiri ni yangu, "Kummbuka siku zote juu ya jambo unalolifanya hata ukiwa peke yako kuwa madhara yake yanaweza kuwa yapi kama jambo hilo litafahamika na umma." Mwisho wa kunukuu. Tena George Bush:"Historia itasema, sisi wote tutakuwatumeshakufa." Sasa ananomasi nani atakukumbuka kwa mtindo wa kujificha huo? Kumbuka kuna mambo huyajui na huyajui au yapo mambo amyo hutayajua na hautayajua kama anavyosema Donald Rumsfield. Kazi kwako kushambia matusi huku unajificha, nani akupe credibility ya kauli zako ukiwa hata wewe mwenyewe huwezi kuzisimamia na kujitokeza wazi?

    ReplyDelete
  8. Mwaipopo, wakati mwingine hakuna haja ya kujibu watu ambao hawaonyeshi kuwa na heshima. Hatutumii blogu hizi kama watu wanavyotumia vilinge vya majadiliano (chat rooms) ambapo kuna kutukanana na kusema lolote lile. Ulingo wetu huu tunauheshimu na sisi wenyewe tunajiheshimu. Lakini pia hatukatazi watu kusema wanayotaka ingawa nadhani sisi hatutakuwa na muda wa kujishusha kwa kuanza majadiliano nayo ambayo hayana mbele wala nyuma. Hasa kama watu wenyewe wanajificha.

    Michuzi: msalimu sana Ras Inno (mwenye kofia kubwa pembeni ya Bob Rudala).

    ReplyDelete
  9. Good job on this event, Michuzi. Hivi una habari yeyote kama this event na ile ya soka were documented on tape or VCD/DVD? Ningependa kuona laivu hizi events kwani wadau wengine tupo nje ya nchi na huwezi kujua what we can changia, especially tukiona what happened laivu. I am willing to buy such events, any events actually, that occur in TZ when I am huku ughaibuni - Sauti za Mwambao, ZIFF, recent Walter Rodney debate kule Mlimani, Yanga vs Simba, Kikwete inauguration etc etc etc.

    ReplyDelete
  10. wewe bwana ndesanjo wacha upuuzi wako hapa,hii ni blogu ya bwana michuzi na ameiweka hapa kwa watanzania wotee,na watu wote wanaotoa michango humu ni kwa ajili isomwe na watu,hivyo mtu anapotumia lugha tusio ifahamu lazima tumweleze ukweli,otherwise
    kama nikwa ajili ya nyinyi tu basi mngekuwa mnatumiana email tu nyinyi kwa nyinyi,au labda ungetuona kwenye blogu yako,lakini no tuko kwenye blogu ya bwana michuzi na tunafurahia sana picha zake kabla hata ya hii blogu, kwenze magazeti mbalimbali tumezoea signature by isa michuzi,
    sasa wewe ndesanjo wacha kujipendekeza kwa michuzi hakuna mtu anaekujua na kwenye blogu zako hatuji ng'o.

    ReplyDelete
  11. Anony, sema 'siji' sio 'hatuji'. Usiusemee moyo wa mtu mwingine. Mbona mimi naenda.

    ReplyDelete
  12. Ni kweli, hata mimi naenda.

    Gawe.

    ReplyDelete
  13. Jamani, katika blogu tunajifunza uvumilivu, na kutofautiana bila kupambana "yaani kuheshimu wale unaotofautiana nao". ni vizuri tukatumia muda mwingi zaidi kuchambua kilichopo badala ya kushambulia watoa hoja.... sioni tatizo la Mwaipopo kutumia uhuru wake kunakshi hoja zake akitumia miundo kauli ya kijijini mwake Kajunjumule!!. pia kimsingi sioni kosa alilofanya Ndesanjo hapa la kumpasa kutukanwa kiasi hiko. kuheshimiana ni jambo la msingi sana. bwana Ndesanjo na Mwaipopo naomba niwaombe msamaha kwa niaba!! mimi huwa ninaenda kwenye world press ya Ndesanjo.

    ReplyDelete
  14. si kawaida yangu kuingilia malumbano, hata kama ya matusi, lakini leo imebidi baada ya kuona mashambulizi kulekea kwa mwana mfalme wetu wa blogu ndesanjo macha. woooote wasemeeni hovyo, ila naomba huyu bwana muacheni. bila yeye tusingekuwa hapa. naungana na mark msaki, ndesanjo, kuomba radhi kwa niaba. naomba usikomee hapo...

    ReplyDelete
  15. Pole sana bwana Ndesanjo ila kama ujuavyo ukubwa jiwe!!!
    Kuna watu katika uwanja huu wa gazeti TANDO wana lengo la sisi washiriki watu katika mijadala hii kua ni wendawazimu na tusio na shughuli za msingi za kufanya bali na MATUSI tu!!!

    Kama alivyosema MARK,kwani tusijenge utamaduni wa uvumillivu na kuheshimiana baina yetu???au yule anayetukana sana katika ulingo huu mwishoni atapewa TUZO???

    Mpaka sasa sioni kosa alilofanya mwaipopo na Ndesanjo hadi kufikia hatua ya kutukanwa kiasi hicho??Hii ni aibu kwetu sote tunaoshiriki bgoguni.Hivi kweli jinsi tunavyoomba viongozi wetu nao wamiliki BLOG kama hizi,siku wakiamua kufungua zao wakute upuuzi wa majibizano na hoja za msingi zinazotolewa na washiriki si watatuona sisi wote tulioamua kuweka majina yetu bila ya uoga wowote nama wafanyavyo wenzetu ni wababaishaji?????

    ReplyDelete
  16. tuheshimiane jamani, heshima ni kitu cha bure, hatuna haja ya kufika huko koote, otherwise tunapaswa kuamsha mada moto zitakazoleta changamoto katika maisha yetu ya kila siku

    ReplyDelete
  17. Wewe Boniphase Makene, Thomas Jefferson na Donald Rumsfield ni wakina nani tena, jamani? Mwaipopo endelea-ga kuandika-ga, na utaeleweka-ga unachoandika-ga wakati wengine wakikisoma-ga kile ulichowandikia-ga! Achana-ga na wakina Boniface Makene wenye kufundishwa-ga heshima kwa miaka mingi. Je, walipewa-ga veti vya heshima kwa kuhitimu-ga? (CHEKENI, na wewe pia Boniphace, CHEKA-GA).

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...