wadau hii imeingia sasa hivi toka ughaibuni. naomba wadau wa mwanza watupe habari zaidi juu ya msiba huu mzito ambao nina uhakika utagusa wadau wengi wa lake

Michuzi,
Habari za Bongo mshikaji.
Kuna taarifa nimepata kutoka huko Mwanza kuwa Mwalimu maarufu katika mji wa Mwanza na vitongoji vyake mwalimu Magadula amefariki dunia mwezi huu huko mwanza.Mwalimu huyu ni maarufu sana kwa wote waliosoma Lake Secondary hata katika forum nyingi wengi walioko nje ya Tanzania lazima watamtaja kila wanapoongelea kuhusu Mwanza.Nimejaribu kuweka katika web ya Atlanta pia hivo nilikutumia hii ili nawe ukiweza tangaza.


Cliff

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. May his soul rest in peace! we will always miss and remember you especially how much we gave you a hard time and you never gave up

    ReplyDelete
  2. aah maskini, ndio hivyo tena, mungu ailaze roho yake peponi amen

    ReplyDelete
  3. Salaam za rambirambi kwa ndugu na jamaa wote popote walipo Mungu amlaze pema peponi amina

    ReplyDelete
  4. Aaaa ni masikitiko makubwa Mungu aifaliji familia yake Amen

    ReplyDelete
  5. Salamu za rambi rambi kwa ndugu ,jamaa na marafiki wote, vile vile kwa watu wote waliosoma LAKE SECONDARY...Marehemu alikuwa mwalimu na mzazi vile vile na mchango wake ulisaidia sana kuiweka LAKE Kama shule.... siyo kijiwe . Mungu amlaze mahali pema peponi AMEN..
    Dr. Balilemwa. B

    ReplyDelete
  6. Mwenyezi MUNGU ailaze roho ya marehemu mwalimu wetu Mr. Magadula, kwani nami nilipitia pale Lake Secondary School na kumaliza masomo ya 'O' Level pale mwaka 1982 na alikuwa ni kama MZAZI wetu aliyetupa kila mtoto alichohitaji hasa kielimu. Naomba pia Bw. Michuzi kama unaweza kunitumia anuani pepe ya Bw. Cliff, maanake alikuwa mwanachama mwenzetu mzuri tu pale NBC Club !!!!! Na kama unaweza mtumie hii blog yangu iitwayo karungula.blogspot.com atanipata kwa habari zaidi.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...