
Hayati Consalva Matanila
Jumuiya ya Watanzania Uingereza inasikitika kutangaza kifo cha Bi. Consalva Matanila kilichotokea jijini London, Uingereza, alfajiri ya siku ya Alhamisi tarehe 2 Agosti 2007.
Bi. Consalva Matanila alikuwa mfanya kazi wa wizara ya mambo ya nje mpaka alipokuja Uingereza kuhudhuria masomo ya elimu ya juu na baadaye akawa mkazi wa London alipoishi mpaka mauti yalipomkuta akiwa usingizini hiyo siku ya Alhamisi.
Bi. Consalva Matanila ana mdogo wake mmoja ambaye anaishi London ambaye ndiye anayeshughulikia shughuli za kusafirisha mwili wa marehemu kwenda nyumbani Tanzania kwa ajili ya Mazishi.
Watanzania wote popote pale mlipo mnaombwa kutoa michango kadri ya uwezo wenu ili kuwezesha kusafirisha mwili kurudi Tanzania kwa ajili ya Marehemu kupumzishwa. Gharama Zinazohitajika ni kiasi cha £2500, na tutaendelea kuwafahamisha maendeleo ya Michango.
Wale watakaoweza wanaweza kupeleka rambirambi zao kwenye Misba:
59 Pitcarne Road
1 Swains House CR4 3LN
au unaweza kuweka mchango wako katika akaunti ifuatayo:
Bank: HSBC
Account Name: Miss. C Kayega
Sort Code: 40-04-10
Account: 01272497
Kuna mbongo mwingine anahitaji msaada jamani.Aliyekuwa mmoja wa wamama hakimu wa kisutu mjini dar-es-salaam.Mama Stella Irene majanjara au kwa jina lingine Salha.Anahitaji msaada wa matibabu hapo mjini uingereza.
ReplyDeletePoleni Jamani wafiwa Mungu awape nguvu kw akipindi hiki kigumu mlichonacho.
ReplyDeleteInasikitisha sana kama kawaida ya misiba, ila kufia ugenini kunasikitisha mno, anyway, watanzania tulioko nje tuungane kwa hali na mali kuhakikisha mwenzetu anaenda pumzishwa kwenye ardhi ya nyumbani.(LEO KWA MWENZIO, KESHO KWAKO).Pole sana kwa wafiwa, mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.
ReplyDeletePoleni wafiwa kwani wote tupo kwenye njia hiyo hiyo. Nimesikitishwa na anon wa kwanza kabisa, kwa kuleta hoja ambayo hapa si mahali pake kabisa. Kama huyo mmbongo mwingine anahitaji msaada basi tujulishane kwa hilo baadae na sio kutumia msiba wa mwenzetu kupitishia agenda ingine. kutoa ni moyo halazimishwi mtu, ila kwa mila zetu za kitanzania wakati kama huu wa msiba ni wakati wa kuwa kitu kimoja na wafiwa na kumuobea marehemu mapumziko mema.
ReplyDeleteTUNGEKUWA NA UTARATIBU FULANI JUU YA HII MISIBA INAYOWAKUTA NDUGU ZETU HASA NYIE MNAOISHI HUKO MAJUU.
ReplyDeleteTUJARIBU SANA KUSAFIRISHA MGONJWA NADHANI HATA BEI YAKE NI RAHISI KULIKO YA KUSAFIRISHA MWILI WA MAREHEMU.
KWANZA MGONJWA AKIFIKA HUKU ITASAIDIA PIA KUWAPA FURSA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI KUMWONA KABLA HAJAFARIKI.
PILI KAMA NINAVYOSIKIA, HUKO MAJUU KUNA VYAMA AU MAKAMPUNI YA WATU AMBAYO WATU HUJICHANGIA KILA MWEZI ILI WAZIKWE ENDAPO WATAFARIKI.
GHARAMA YAKE NASIKIA KWA MWEZI NI SAWA NA KUNUNUA KOPO MBILI AU TATU ZA STELLA AU FOSTERS.
SASA KIPI BORA, KUNYWA STELLA NA FOSTERS KILA SIKU AU KUTOA MCHANGO ILI UKIFA UWEZE KUHIFADHIWA MAHALI PAZURI? POLENI WAFIWA, TUOMBE MUNGU HUYO MWINGINE ANAYEUUGUA NAYE APONE.
We anony 8:34 hapo juu, Grow up..nadhani wewe ndio huyohuyo uliyeweka ujumbe wako kwenye msiba wa mzee wetu aliyefia marekani, eti kuna hela unaweka kila mwezi ili ukifa upate msaada, wacha hizo, na kusema mtu asafirishwe kabla hajafa, watu wanahangaikia roho za wapendwa wao mpaka dakika ya mwisho..hemu wacha ujinga, we uko bongo UNAPENDELEA ZAIDI MICHANGO YA HARUSI NA MINGINE INAYOHUSIANA NA KWENDA KULA LA KUNYWA, ya kusafirisha marehemu unaona kazi,,na hapo wala hutegemewi kutuma hela yako huku kusaidia kitu, so SHUT UP.
ReplyDeleteNapenda kuchukua fursa hii, kutoa shukrani kwa wale wote waliojitolea kwa hali na mali kufanikisha mazishi ya mpendwa wetu, mama yetu, mlezi wetu Marehemu Consalva Michael Matanila.
ReplyDeleteMungu awazidishie pele pote mlipotoa apaongezee.
Mbarikiwe sana, Raha ya milele umpe eebwana na mwanga wa milele umwangazie, astarehe kwa amani amina.
Matanila Family DAR
Jamani Dada, tulikupenda sana!!! lakini Mungu alikupenda zaidi. Ulikuwa mlezi wa familia na ukoo wote!!. Tutakulipa nini sisi dada!! Kila ukiombwa msaada wa kazi, elimu, chakula, mavazi neno lako ni moja tu sawa nitakusaidia, nitakusomesha, nitakununulia nguo, nitakutafutia kazi, kwakweli pengo lako halitazibika kamwe. Tunalia, tunasali tunakuombea dada, ulale pema peponi, mwenyezi mungu akupumzike pumziko la milele.
ReplyDeleteUa lililo chanua limenyauka. Kaka yako Mpwendwa Plasdius Michael Matanila, alikuwa kila siku akikukumbuka presha juu! mwisho baada ya miezi mitatu tu naye akaaga dunia!! jamani ni machungu juu ya machungu.
Sisi sote tumemuachia mungu yeye ndiye anayejua. Faraja ya kutupa sisi wadogo zenu.
Mlale pema peponi. Raha ya milele huwape eeee bwana na mwanga wa milele huwaangazie.
wapumzike kwa amani - Amina.
Tarehe 02/08/2007
ReplyDeleteKamwe hatutaisahau! Giza zito lillingia ndani ya familia yetu, kuondokewa na Malkia wetu, taa yetu, tunakukumbuka sana familia ya Matanila!
RIP Consalva Matanila, Dada Mpendwa!!!