
wadau toka kulia: mussa shila, benedict bosco na christopher mashingo na mazoea kundayo wakiwa wamejipanga tayari kupokea nondo zao za mastaz kwenye biashara na uhasibu toka kwa gavana wa jimbo la missouri baada ya kuhitimu hivi karibuni chuko kikuu cha missouri state university (www.missouristate.edu) katika kuendeleza libeneke la elimu. kundayo kala nondo ya biashara na fedha.
aidha, nasikitika kusikia kuna baadhi ya wadau ambao wanachukia kuona vitu kama hivi katika globu hii ambayo ni ya kila mmbongo. kwa upande wangu mie sina neno hasa ukizingatia kwamba mie mwenyewe darasa iz noti richebo hivyo huwa naona furaha na fahari kuona wabongo wanapiga bao umande. kunradhi kwa wote wenye mawazo tofauti ila naomba mniruhusu kuendelea kupokea snepu kama hizi ambazo ni changamoto nzito kwa jamii yetu inayostrago kwenye elimu dunia...
hata hivyo nitakuwa mtovu wa adabu endapo wadau wanaolalamikia picha kama hizi nitawabeza, hasa kwa kuwa wengi wametoa wazo mbadala kwamba tutenge siku moja ya kubandika picha za nondozzz. nami naafikiana nao na naomba idhini kuchagua siku hii ya jumatano kufanya hivyo. kwa maana hiyo basi kila mwenye kutaka picha yake ya nondozzz ibandikwe anitumie wakati wowote pamoja na maelezo kamili ila nitakuwa naibandika siku za jumatano tu. kila upande naomba uelewe kwamba nawaheshimu na kuwapenda sana wadau wote hivyo sina ubavu wa kupendelea upande mmoja. nahisi mmenielewa na kila upande utavuta subira. anuani ni ile ile issamichuzi@gmail.com
Michuzi acha utani, caption zako kwenye dailynews huwa hujichanganyi zimenyooka safi, sasa hapa mbona unachanganya neno blogu na globu
ReplyDeleteKaka michuzi bwana kwa kujifanya hajasoma cardiff ulienda kufanya nini au sijui liverpool.ni vizuri kuwa muwazi kuhusu elimu yako pia ni changamoto kwa watu wengine. maana watu wajue mafanikio ya wengi ya maisha pia yanachangiwa na elimu kama wewe ulipofikia na kuheshima na kusoma ni wakati wowote hakuna aliyechelewa kuna mama sijui nchi gani nimeona kwenye TV ana kama miaka 93 amepokea Masters.huo nimtazamo wangu
ReplyDeleteLizzie
Michuzi, nashauri ikiwezekana weka kila siku picha za wanaopata nondozzz.Inasaidia kuwapa changamoto wale waliamua kuacha shule na kuendeleza libeneke la kubeba mabox.Nafikiri unafahamu Wengi wanaotoka TZ wanaanga wanaenda shule, wakifika huku wanaweka shule pembeni,na kuingia street kufanya shughuli nyingine na ndio hao wanaochukia wanapoona wenzao wanapata nondozzz.
ReplyDeleteMichuzi Mkuu wewe weka Nondozz kadiri unavyozipata, kuna misimu ya graduatiosheni utaziona sana kwa hiyo wewe ziweke tu usizitengee siku bwana. Wasipenda watatuwia radhi. Kwa kweli picha za Nondo hupendeza sana, mie mwenyewe nawaonea wivu hao jamaa wanaopata nondozzzz lakini sio wivu wa kijinga hadi kuchukua kuona picha zao.
ReplyDeleteSijawahi ona picha ya Nondozzz ambayo sio nzuri kusema kweli na watu hao huwa wote wana furaha kwenye picha zao, kwa kweli huonekana vizuri sana.
WEKA masnepu ya nondozzz enetaimu, anedei, enewea.
michuzi Snepu za nondozzz ndio zenyewe, zinaleta changamoto kwa sie tusio kuwa na shahada. so wewe weka tu bila kupanga siku maalum, wasiotaka ujue shule is not for them ndio maana hawatasaki kuona progress za wengine.
ReplyDeleteMi sioni sababu ya nondoz kuwekewa siku yake. Ina maana basi kila kitu kiwekewe siku yake, sasa kutakua na uhindo wa blogu kweli? Blogu ni mchanganganyiko wa picha na habari mbalimbali, hakuna kuchagua sijui J5 nondo sijui J4 mbaoo..!
ReplyDeleteMichuzi usiwasikilize wenye wivu. Kwanza ni jitu moja tu linalojiita PhD holder ndilo linalochukiaga nondo za watu.
Weka nondo na sisi tuwe inspayadi.
Kaka michuzi najua unataka kuwafurahisha wadau wako wote wanaotemebelea hii blogu, kitu ambacho hutaweza kufanya. Wewe kama mwandishi wa hii blogu ndiye mwamuzi mkuu wa mambo utakayoyaweka humu ndani, ukianza kufuata matakwa ya kila mdau utachanganyikiwa. Kwahiyo watu wasikupangilie nini kiwekwe humu ndani ama kwa siku gani kuwe na jamoi flani, maamuzi hayo ni yako pekee. Kama hawataki kuangalia picha za nondo basi wasiiangalie, kwani wamelazimishwa. mimi sioni ubaya wa kuweka picha za wadau wako wakipokea nondo, na kama ulivyosema mwenye ni motisha kwa vijana wengine. fanya kazi yako as you see fit kaka michuzi...let the hater's hate.
ReplyDeletePapaa Nzuwa Mkende...izaa ibee umekamata gamba lako si mchezo. Mbona hukutualika kwenye sherehe?Sasa unapanda daarini ?(Ph.D) Safi sana.
ReplyDeleteHongereni Sana mliograduate, watu wasiopenda picha za nondozz bila shaka ni watu waliokimbia umande na wasiopenda maendeleo ya wabongo wenzao , hivyo nakuhisi michu uwa-ignore watu kama hawa kwani ni watu wanaosababisha kudidimia kwa uchumi wetu! Hivyo basi ni bora uendelee kuziweka picha hizi kama kawaida na hakuna haja ya kuzitengea siku maalumu, kwani kwa mfano picha za harusi au sherehe nyingine je zina siku maalumu ya kuziweka?
ReplyDeleteWanaopinga nondoz snepu, hawajui umuhimu na furaha ya kumaliza shule in other words sio waenda shule. conclusion: Michuzi tupe snepu hizo anytime,anyday watu tupo vyuoni tunapata stimu za kumaliza haraka alaaa, hao wanaokwepa umande shauri zao. Kuna jamaa kanifurahisha sana kwenye comments zake eti bongo kama Newyork skuiz, magari makali,mara maleksuz,ieksi,maskyscraperz,manyumbaz na watu wanaishi kama mamtoni!!! hahahaa ngoja tu graduate watu turudi home is homez!!!
ReplyDeletewakaka hongereni sana hayo ndio maendeleo kukamata nondozzzz. wanaomia kuweka snep za nondo ni kwamba hawana snep zao za nondozzz sasa michuzi nasema hivi tuwekee snep anytimu mpaka hao waliokimbia umande wapande stimu.
ReplyDeletekuna kaka mmoja hapo tulukuwa naye jefferson city huyo wa pili alikuwa mchafu sana bafu lake lilikuwa na funza wengi sana mpaka landlord akamtimua, huyo wa mbele anaonekana mpole kweli.
ReplyDeletewe anonymous unayezungumzia uchafu wa mwenzie sidhani kama hili ndio eneo lake ulipaswa kumueleza wakati huo sasa hivi haihusu mpe hongera zake mwenzio kashika nondo yake. we hatujui una nini??!!
ReplyDeletemichuzi we tuwekee snep za nondozz enitaimu achana na wajinga wajinga wenye wivu wa maendeleo.
ReplyDelete