Familia ya Mchungaji Vincent Joseph Chacha wa Bukoba, Kagera, wanasikitika kutangaza kifo cha kijana wao mpendwa Philemon(BHOKE) Vincent Chacha (pichani) kilichotokea tarehe 17 mwezi 3- 2008, huko Durban, Afrika kusini, baada ya kuugua ghafla siku ya Ijumaa .
Mipango ya kusafirisha mwili wa marehemu kwa ajili ya mazishi kutoka Durban Afrika ya kusini inafanywa na ndugu, jamaa na marafiki.
Bwana aliyemtoa ndiye huyo huyo aliyemtwaa, jina lake libarikiwe.Amina
Joseph Wambura Chacha
Kaka wa marehemu

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Bwana alitoa, na Bwana ametwaa; Jina la Bwana libarikiwe. Amen.

    ReplyDelete
  2. NAPENDA KUTOA POLE ZANGU KWA FAMILIA YA VINCENT CHACHA KWA MSIBA ULIO WAKUTA WA KUPOTELEWA NA KIJANA WAO MPENDWA BHOKE,NI KIJANA NINAE MFAHAM TOKEA ALIPOKUA MDOGO WAKATI TUNAISHI JIRANI PALE UBUNGO KIBANGU,KIFO CHAKE KIMENISIKITISHA SANA KIASI NINASHINDWA KUAMINI.MUNGU AIPOKEE ROHO YAKE NA AIPUMZISHE KWA AMANI, AMINA.MDAU LONDON.

    ReplyDelete
  3. Nipo nyie katika kipindi hiki kigumu kwenu cha majozi ya kuondokewa na ndugu yetu ila tukumbuke kwamba mbele yetu nyuma yake apumzishwe kwa amani

    katochi)

    ReplyDelete
  4. SOTE NJIA NI MOJA YEYE AMETANGULIA SISI TUTAMFUATA, MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA PEPONI.

    ReplyDelete
  5. ni masikitiko sn kijana mimi simjui ila baba yake nina mjua na ndiye aliyeniambia taarifa hizo pale bandarini bukoba siku anatoka bk kwenda mazishini musoma. RIP

    ReplyDelete
  6. Pole zangu nyingi kwa Mzee Vincent na Familia yake.Ndugu zake tulioko hapa Dar tumejitahidi kiasi tulichoweza kuhakikisha mwili wa Marehemu Bhoke unaletwa nyumbani kwa mazishi.Shukrani za pekee ziwaendee Mzee Madebe,Cyprian Mwita(Toye),Marwa Magumwa,Mzee Pius Mabuba na hasa Baba Mdogo wa Marehemu Mr Philemon Bhoke Joseph ambaye ameisimamia vizuri shughuli hii nzito.RIP

    ReplyDelete
  7. Natoa pole zangu nyingi sana kwa familia ya Rev.Vicent Chacha kwa msiba huu mkubwa wa kumpoteza kijana wao mpendwa.Tunamuomba Mungu baba aipumzishe roho ya marehemu mahali pema peponi Amen.MC.

    ReplyDelete
  8. Nimesoma habari hii kwa mshituko mkubwa sana! Ni miaka mingi imepita bila mawasiliano na familia ya Mchungaji Chacha. Katika kutafuta km naweza kupata taarifa yoyote online ndo nakutana na habari hii ya kusikitisha.

    Nimekua na Bhoke na kuabudu naye kanisa moja (Musoma) na ninaposoma habari hii inaniwia vigumu kuamini!!

    Naipa pole familia ya Mchungaji wangu, Mchungaji Chacha kwa msiba huu. Mungu na awatie nguvu!

    Mr. Bwire Ally
    (Dar es salaam)

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...