Waziri Mkuu Mh. Mizengo Pinda akizungumza na Mwenyekiti na Mkurugenzi Mtendaji wa RITES ambaye pia ni Mwenyekiti wa Shirika la Reli nchini (TRL), Vinay Agarwal ofisini kweke jijini Dar es salaam. Shirika hilo limekumbwa na mgogoro kwa wafanyakazi kugoma kudai mishahara mipya na mambo kadhaa mengine. kwa habari kamili bofya hapa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. I dont know, if this is happening in our country, but I just want to add to this topic, we should have legislative process demanding these foreign investment companies and other public companies releasing their financial files quarterly/yearly like many other countries in the world.


    By Mchangiaji.

    ReplyDelete
  2. Kuna umuhimu wa wafanyakazi wa Reli kuongezwa mshahara kwani kazi zao ni ngumu na kipato chao ni kidogo sana. Hata huu wa 160,000 (USD 150) bado ni mdogo sana. Kitu kinachoniudhi kwa wenzetu wenye ngozi nyeupe ni kitendo cha kutufanya sisi weusi kama siyo binadamu na hatustahili kuishi maisha bora, mara nyingi mswahili anaweza kuwa na taaluma kubwa lakini analipwa kidogo na mhindi (mfano) analipwa juu japo hana taaluma kubwa na ukiuliza hapa utambiwa life style ni tofauti au sisi wahindi huwa tunasaidiana kwa style hii. Nadhani huu ni wakati wa kupigania heshima yetu baada ya wazee wetu kuwaondoa wakoloni la sivyo weusi tutakuwa tunajidharaulisha wenyewe hasa ukizingatia kwamba haya mambo yanatoke katika nchi zetu. Hivi sisi tumezaliwa weusi ili tuwe watumwa wa hawa weupe au wenzetu wametuzidi ujanja tu kwa kujithamini wao wenyewe, tamaduni zao na kila kitu cha kwao huku wakitudharau sisi pamoja na tamaduni zetu na kibaya zaidi weusi wenzetu wanatumika kutumaliza. Tufanyeje?

    ReplyDelete
  3. Pinda kwa ukaaji huo, sisi wataalamu wa facial expression naona umeridhika na anachokuambia huyo jamaa. Zaidi yake unaonekana unamuonea huruma asilipe hiyo 160K. Wadau nisaidieni kuhusu hilo.

    ReplyDelete
  4. Kapuya azomewa TRL

    2008-04-04 08:47:01
    Na Raymond Kaminyoge


    Wafanyakazi wa Shirika la Reli Nchini (TRL), wamemzomea Waziri wa Kazi, Ajira na Maendeleo ya Vijana, Profesa Juma Kapuya na kugoma kusitisha mgomo hadi watakapopewa tofauti ya mishahara yao na siyo ahadi.

    Waziri Kapuya, alikwenda kuwaomba wafanyakazi hao waliogoma tangu jana na kukusanyika katika Karakana ya TRL, jijini Dar es Salaam kuendelea na kazi wakati serikali inashughulikia suala lao.

    ``Hatutaki siasa hapa, tunataka fedha zetu, kama hujaja na fedha tafadhali rudi ofisini ukaendelee na kazi nyingine ya kuwahudumia wananchi, tukipewa sehemu ya mishahara yetu ndiyo tutaeendelea na kazi na si kukalia politiki,`` alisema mmoja wa wafanyakazi hao.

    ``Mbona hivi karibu nyie Wabunge mmeomba kuongezewa mishahara na mmekubaliwa iweje sasa serikali ifanye mzaha na maisha yetu, wananchi watusamehe, hatutatoa huduma ya usafiri hadi tutakapopewa fedha zetu,`` alisema Bw. Masindiko James.

    Hatua hiyo ilikuja baada ya Waziri Kapuya kuwaomba wafanyakazi hao kuendelea na kazi na kuahidi kuwa serikali itafanya ukaguzi wa mahesabu ya TRL ili kuona kama mwekezaji huyo anapata faida au hasara.

    ``Serikali inawaomba mrejee kazini, tunaunda kamati itakayochunguza mahesabu kwa wiki moja, ikithibitika kuwa kampuni haina uwezo wa kulipa nyongeza serikali itatafuta fedha na kuwalipa sehemu ya mishahara yenu,`` alisema na kuongeza kwamba serikali kwa sasa inachukua dhamana ya fedha hizo.

    Aidha, Waziri Kapuya alisema serikali kwa kushirikiana na uongozi wa TRL wataangalia vyanzo vingine vya kupata fedha ili kuongeza uwezo wa kampuni hiyo ili iweze kulipa mishahara mipya pamoja na malimbikizo kuanzia Machi.

    ``Nawaomba wafanyakazi mrejee kazini mkawape huduma wananchi wanateseka kwa kukosa usafiri suala lenu tunalishughulikia na fedha zenu mtalipwa,`` alisema Waziri Kapuya.

    Licha ya wafanyakazi hao kuombwa mara kadhaa na Waziri walikatiza hotuba yake mara kadhaa kwa kumzomea huku uongozi wa TRAWU ukifanya kazi ya ziada kuwanyamazisha ili wamsikilize Waziri.

    Wafanyakazi hao walisema wanashangazwa na suala hilo kutatuliwa kisiasa wakati makubaliano ya kuongeza mishahara yalifikia makubaliano baina ya pande zote tatu TRL, TRAWU na wizara ya Miundombinu.

    ``Tueleze Waziri hawa wahindi wamewapa nini mpaka wanakiuka makubaliano ambayo wameyasaini wenyewe mbele ya serikali,`` alisema mfanyakazi aliyejitambulisha kwa jina la Julius.

    Alisema shirika hilo limepandisha nauli za abiria pamoja na mizigo na kupunguza wafanyakazi hali ambayo wanaamini imeliongezea shirika kipato.

    ``Mwekezaji huyu hana alichowekeza, vichwa vya treni alivyoleta ni vichakavu, anapata faida kwa kutumia miundombinu yetu, kwanza alivyo jeuri hata kwenye mkutano huu hajaonekana, wanajivunia nini wahindi hawa?`` Alizidi kuhoji.

    Baadhi ya mabango yaliyowekwa na wafanyakazi hao mbele ya Waziri Kapuya yalisomeka: ``Kapuya hii siyo Akudo``, ``Kapuya wahindi wamekupa nini?``, ``Serikali inathamini wahindi kuliko wapigakura``, ``Hii ni Tanzania au tuko India?`` na ``Mkapa wachukue wahindi hawa wapeleke Kiwira``.

    Wakati wafanyakazi hao wakiendelea na mgomo, wasafiri waliotarajia kusafiri na treni walikuwa wamekusanyika katika makao makuu ya TRL wakisubiri hatma yao na kufuatilia mgomo huo kama utaisha ili waendelee na safari.

    Mwezi uliopita wafanyakazi hao waligoma ili kushinikiza uongozi kuwapa nyongeza za mishahara.

    Mgomo huo ulimalizika baada ya uongozi TRL kukubali kuongeza mishahara ya kima cha chini kuanzia Sh.160,000 badala ya Sh. 87,000 walizokuwa wakilipwa ambazo zingeanza kulipwa mwishoni mwa mwezi uliopita.

    Hata hivyo, mwishoni mwa mwezi wafanyakazi hao walishangaa kulipwa mishahara ya zamani hali iliyoanzisha mgomo mwingine ambao unaendelea leo.

    SOURCE: Nipashe

    ReplyDelete
  5. Hapo ni meeting of the unequal. Pinda yuko serikalini maisha yake yote, huyo mhindi ni mfanya biashara mahiri na alitetoka kwenye mazingira mgumu zaidi kibiashara kama India, miono yao ya dunia ya kibiashara na maendeleo ni tofauti sana...unafikiri hapo kuna kitu?

    Mdau unayesema hatujithamini ni kweli: Wenzetu kwao wanajipendelea wao, sisi kwetu tunawapenelea wao.

    Nasikia huyo wa Botswana anayewekeza Mlimani project anakataa kuendelea anataka misamaha zaidi ya kodi na upendeleo zaidi!!! Ujumbe mzito ulikwenda kumuona KWAO Botswana. Yaani hakuna wawekezaji wa KiBongo wanaoweza kufanya huo mradi???

    Hebu mchukue Mengi, Ali Mafuruki na wengineo uwape huo mradi na upendeleo wote huo uone watakavyofanya kazi nzuri. Ndio, lazima serikali iwe na uwezo wa kuwapendelea waTanzania. Mnafikiri nchi hiiitajenwa na wasio waTanzania? Hata kilimanjaro tulimnyima mzawa Mengi.....

    ReplyDelete
  6. Huyu mkurugenzi anakutana na waziri mkuu face to face, je na mwakilishi au wawakilishi wa wafanyakazi wa kampuni hiyo nayo anapata fursa ya kujadili mgogoro huo face to face na waziri mkuu???Kesi haiwezi kusikilizwa upande mmoja!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...