Mdau Michuzi
nampa pole sana dada Jovinata kutokana na yaliyomfika.

Kwa mawazo yangu, tukio hili ni moja ya mengi yanayoakisi matunda ya jamii yetu, kwamba si sote wenye upeo wa mawazo mazuri kutokana na ama uchache wa elimu au kutokuelimika.

Lakini pia nadhani inabidi tuwe na tahadhari pale tunapokusudia kufanya mambo mbali mbali, na tujiulize kama jamii yetu tayari imeelimika kiasi cha kutosha kuendana na lile tunalotaka kulifanya.
Nasema hivyo kwa maana kwamba utamaduni wa uwazi bado ni mgeni sana kwa jamii yetu, japokuwa katika nchi za Ulimwengu wa kwanza tayari ni sehemu ya maisha ya kila mtu. Kwetu hatukuzoea haya mambo ya kutangaza sifa za mchumba umtakaye, na huu ni ukweli lazima tuukubali.
Sasa inapotokezea watu kuanza kukushushia matusi, nadhani hilo ni somo na wakati mwengine inabidi uvumilie na kumeza mate ya uchungu. Lakini pia huna budi, kama mwana jamii, kabla ya kuwasiliana na jamii yako ufanye homwak ya kutafakari namna jamii itavyokupokea.

Wakati mwengine kuiga maendeleo kwa maana tu ya kuiga kuna athari yake, kwani jamii uliyomo haijafikia pale unapoifikisha.

Lakini isiwe na maana kuwa tusipeane mawazo na maoni kuhusu tuyafanyayo. Nakumbuka niliwahi kutoa maoni yangu binafsi Manka alipotoa tangazo lake la kutafuta mchumba. Bahati mbaya mawazo yangu yakapotelea kapuni.
Niliamini hayakuwa na negative yoyote, lakini labda mhariri hakuamini hivyo, maana hiyo ilikuwa mara yangu ya kwanza maoni yangu kutotolewa ndani ya blog.

Tunapokosoana na kushauriana ni vyema pia sauti zetu zikasikika, na labda hilo litasaidia kuepusha wenye matusi kuacha matusi yao na kushawishika kuiga ustaarabu wa lugha nzuri.

Vinginevyo, labda ukimya huchochea ukorofi.

Pole sasa dada Jovinata, na Mungu atasikia dua yako, na utafanikiwa kumpata mchumba umtakaye.
K Sahal,
Leicester

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 15 mpaka sasa

  1. sasa huyu jamaa amekuja kuongea nini? nimejitahidi sana kusoma kwa makini lakini sijapata ujumbe alokusudia

    ReplyDelete
  2. Huyu nae kaongea pombe ya kichaga ja jana/ngela! haaa, mnadai exposure ndo inasaidia watu kuelewa mambo, I cant buy that, maana waliomtusi huyu dada wako tz na nje ya Tz, so kutoka nje ya nchi hakumwongezei mtu ustaarabu, au wingi wa madarasa haukupi utu! utu ni wewe mwenyewe, regardless una miaka mingapi ya kukaa darasani. Thats my 0.02 cents!

    ReplyDelete
  3. @ any April 4, 13:00 PM EAT.
    He is a liberal! always confused, no clear message. May be I can help.

    Ujumbe tuache matusi, na dada Jovinata should have played it low, finding a perfect man through conventional method rather than world wide web, like mmhh?? check out on your neighbor, working mate, or even asking your father for a tip or two, since your mother is not with you, may she rest in peace.

    Seriosly, Dada Jovinata, you should relax a little, have a chit chat with few men out there, and you will definitely find someone who match your credentials, always open up this idea with your father/married brother, inviting him for a dinner TRUST me it works wonder, you will find the honesty of a man with a FATHER/BROTHER PRESENCE. Additional to that, once you have passed this process, let him chat up with your father/brother alone, and trust me again on this they will give you a perfect description of the mchumba wannabe charater, let them know each other. I am sure they will give an honesty and candid answer, if they UNDERSTAND.

    I wonder how did you end up dating a married man of two wives. Just be careful out there, you are falling victims for your own good. The other way around is to get an advice from a married woman, like your friend, auntie, neighbor or a co worker, you will pick up a lot experience from them, ie their personal stories, how to get over a bad relationship and so on, how to treat a man and so on. WARNING THIS IS A TRICKY process, if you know what I am talking about, there are limits or you will end up, your best friend dating your mchumba wannabe. BE careful with your words and blank cheque situation, play your ball rather careful. You girls you know what I am talking about. I am sure you are smart enough to overcome that.

    Anyway, WISH YOU ALL the best on your quest for a perfect man.

    By Mchangiaji

    ReplyDelete
  4. Kwa kifupi alichosema huyo kaka hapo juu ni kuwa duniani kuna watu na viatu. Na asiyefunzwa na mamaye ulimwengu utamfunza. Hao wanaotukana wenzao kwenye blogu kuna siku watafunzwa na ulimwengu. Ingawa amezunguka sana lakini ni hayo ndiyo aliyoyalenga.

    ReplyDelete
  5. watanzania wengine haswa wale washamba, kufwatilia maisha ya watoto wa watu, utawajua kama mtu amesema ivyo si anahitaji masaada, basi wengine hata nje ya nchi wanachukulia vingine, wivu na chuki, muwe na moyo wa kusaidia wenzenu acheni chuki, watanzania.

    ReplyDelete
  6. Mchangiaji na wengineo mnaomshauri Jovinata atafute mchumba hapo alipo, ameshasema yeye yuko Sudan kikazi sikumbuki jina lakini yuko bush, sasa huko atampataje? Na inawezekana hata huyo mume wa mtu alimpata kwa mtindo huo huo wa unaomshauri aufuate.

    Nyie wanaume hili suala mnaliona mzaha kwa kuwa kwenu si kazi kupata mchumba ni suala la kuamua na kuchagua yupi umtakae. Lakini kwa mwanamke inabidi asubiri mpaka atokee mtu wa kumchagua na wakati mwingine ndio hivyo anatokea mtu ambaye ni mwongo na mlaghai, mume wa mtu! Sasa mlitaka afanyaje? Mbona kutaka mchumba ni suala la kawaida tu, tena liko simple. Kwa yule ambaye hakuhitaji mahusiano na Jovinata hakuwa na haja ya kumtumia email yoyote seuze ya matusi, na yule ambaye labda alijiona ana sifa au anakaribia sifa alizotaka angetuma email kwa Jovinata.

    Ninachojua kuwa watanzania ni abusers! wamezoea kuabuse watu kwa namna mbali mbali na hasa privacy ya mtu ingawa hapa mtasema ameweka email address yake, pamoja na hayo hakusema watu wamtumie email za matusi. Hii inaonyesha jinsi watu walivyo SICK! SAIKOLOGIKALLY SICK! ABUSERS! Wanapata raha fulani hivi wakim abuse mtu! Hawa kwa kweli wanahitaji tiba. Na tiba yao iko njiani siku watakapofikishwa mahakamani kwa matusi ndio siku watapona huo ugonjwa!

    ReplyDelete
  7. I still don't know where am i standing? coz the way i consume and digest this looks way far fromsome wadau waliopata exposure.

    nimetembea nchi tofauti duniani na sasa niko USA, nimekutana na watu kutoka sehemu nyingi na nchi nyingi tofauti, lakini kila mmoja alikuwa proud of what and who he/she is esp. traditionally.

    Kuna watu akiwemo michuzi wamesema haya ni maendeleo, ila mimi nina swali moja kwa hao wenye maendeleo je kwa nini watu wenye tamaduni kama za Jovi "sorry Jovi" nchi zao kiwango cha divorce ni kikubwa ukilinganisha kwa sisi wabongo wachache "washamba"?

    ReplyDelete
  8. Tatizo bado swala la mapenzi hatujaripa kipao mbele mi nachoweza kumshauli jovinata amtafute mtu watayependana kwa dhati na sio vigezo vya darasa mbona kunawatu kibao ambao wameshia darasa la saba na wanamaisha mazuri kuliko hao walio soma kuwa huru na mwenye furaha na umpendaye akupendae kuliko gereza la vigezo

    ReplyDelete
  9. Nimesoma maelezo ya wanablog wengi na maoni yao, kweli kero zimezidi jamani. WATANZANIA wenzangu tubadilike, anachoeleza mlalamikaji juu ya kutusiwa kwa Jovita kwa upande wangu ni sahihi kwani hakuna sababu ya wewe kumtusi mtu pasipo sababu ya msingi.

    Na kwa upande mwingine naweza kusema kweli bado elimu ya utandawazi hatujaielewa vilivyo kuliko. Ndiyo maana mtu anafyatua matusi kwenye Mtandao huu akifikiri kwamba mtu aliyetuma maoni yake kutafuta mchumba au kingine ni limbukeni, hapana ndugu yangu, hii ni njia rahisi ya kupunguza Gharama zisizo na msingi kama vile kumpigia simu mtu ambaye ungependa uwe naye.

    Kwa njia hii ujumbe unawafikia wengi na yule ambaye atajikuta kiatu hiki ni saizi yake basi akivaee, nikiwa na maana kwamba kama atapendezwa na kuvutiwa na mtumaji wa maombi basi afanye naye mawasiliano, hasa hii desturi ya kutusiana kwenye blog hii inaonesha uduni wetu wa Elimu ya utandawazi na namna nzuri ya kutumia mitandao.

    Ujumbe tu ache lugha ya matusi ikiwa kiatu ni saizi yako kivae na kama siyo achia wengine.

    ReplyDelete
  10. Nimechunguza mara nyingi wanaokuwa wa kwanza kutoa maoni yao humu aghalabu huwa wanaongea kwa jazba na munkar au wanaongea pumba (vapour), ushauri wangu unapomaliza kusoma habari jaribuni kutafakari kidogo sio kuruuuka na jazba zisizo na manufaa.

    Jamani hichi ni kijiwe cha duniani hapa, na unaweza kuzunguka dunia nzima kwa ncha ya vidole vyako hiyo ni afadhali sana, maana tunaelewa mambo mbalimbali humu na tunajifunza vitu mbalimbali, tunatiana moyo, na tunafarijiana. Isiwe na kutukanana jamani haipendezi. Mimi siamini kama kuna mzazi huwa anamfundisha mwanae matusi au kuwa mtu mbaya huwa tunafundishwa maadili na tabia njema tangu wadogo mama huwa mkali sana mtoto anapotukana au hata kufyonza mtu , hiyo ni moja ya masomo tunayopata nyumbani, dhumuni tunajengwa tuwe raiya wema wenye heshima na adabu. Sasa mtu akija hapa na kuongea upotovu au kutovukwa(utovu wa adabu) humu, inatuonyesha yale maadili aliyokuwa anapewa akiwa mdogo walikuwa wakifanya kazi ya bure hakuwa msikivu. Kuna neno linasema mtu hunene yamjazayo moyo, na unapokutana na mtu ile pyeeee kumuona tu huwezi kumjua ni mtu wa namna gani subiri afungue mdomo wake hapo utasema huyu wawapi, hata awe kichwa kimejaa mvi utamjua tuu busara zake ni kiwango gani tabia zake ni za watu gani.Nawaomba ndugu zangu tuwe mstari wa mbele kuwasaidia vijana tunaowazidi hasa kwenye mambo ya kifamiliam iwe anaataka kuanzisha au ameshaipata tuwe na roho ya kutoa msaada endapo utahusishwa, hata Mungu atakuwa amefurahishwa nawewe.

    Namalizia kumpa Pole dada Jovi kwa maneno magumu yaliyomuumiza roho, aidha kwa dhihaka, au kwa kejeli, hii ndiyo dunia, sipendi kukwambia mengi, hapa ndo unatafuta MCHUMBA vita kama hii, na ukishampata ndo usiseme mdogo wetu, kuna watakaofurahia na watakaochukia, na watakaotaka kukuharibia na watakaotaka kukuchukulia, Mwaya KUWA UJIONEE.

    ReplyDelete
  11. Hivi majina haya jovinata yanatoka wapi?

    ReplyDelete
  12. Nakubaliana na wadau wanaopinga matusi katika blog "yetu" ya jamii.

    Naomba nitoke nje ya mada kidogo!!

    Huwa napata shida sana kusoma "paragraph" (kimatumbi hapa kapa) ndefu au kwa lugha nyingine, paragraph zenye zaidi ya mistari nane (my standard). Natumai hili ni tatizo kwa wadau wengine pia.

    Natoa ombi kwa wale wanaoandika paragraph ndefu wazifupishe. Njia rahisi ya kufanya hivyo ni kuandika "idea" moja au mbili kwa kila paragraph. Hii inasaidia kufikisha ujumbe kwa urahisi na kuvutia msomaji.

    Ignorant,
    Jeremani

    ReplyDelete
  13. KUTOKANA NA JINSI ALIVYOJINADI DA JOVI INAONEKANA KABISA KUWA HAJAWAHI PATA EXPOSURE YA KUWA KARIBU NA WATU WA AINA MBALI MBALI(KITABIA).

    KWANZA ANGEJIULIZA KATIKA WADAU ZAIDI YA MILIONI TATU NA NUSU HUMU KIJIJINI (BLOGUNI) WANGAPI WANA SHAHADA YA KWANZA LICHA YA HIYO YA PILI. PIA NINGESHAURI KUWA TUJIFUNZE KITU KINACHOITWA FLEXIBILITY!, KWA MFANO, INAONEKANA ALIMZIMIA SANA KAKA MASHAKA, JE MASHAKA NI WA DHEHEBU LAKE NA KAMA LA... ATAFANYAJE.

    TABIA YA MTU MARA NYINGI INATOKANA NA MALEZI ALIYOYAPATA KATIKA MAKUZI YAKE. HATA KAMA KUNA SOMO LINALOITWA TABIA SHULENI, BASI MWANAFUNZI ATAJIFUNZA TU ILI MRADI AFAULU MTIHANI!

    TAFITI ZINASEMA BINADAMU ANA UWEZO WA KU-PRETEND HADI/KATI YA MIAKA SABA HADI KUMI, KWA MAANA HIYO BASI, KUNAUWEZEKANO PIA WA KUKUTANA NA WATU WA AINA HII ESPECIALLY TUKIWA SO DEMANDING!

    NINAMUUNGA MKONO MCHANGIAJI, KWAMBA DA JOVI AJARIBU KUPIGA MBIYU TU KWA WATU WAKE WA KARIBU KAMA VILE BABA, KAKA, SHANGAZI, MARAFIKI NK (USIWAONEE AIBU AU KUWAOGOPA HAO NDIO WA KUKUSAIDIA ZAIDI...!) , NINA UHAKIKA KABISA WATAJIPANGA WENGI TU HADI MWENYEWE ATACHANGANYIKIWA.

    BEST OF LUCK DA JOVY

    ReplyDelete
  14. watanzania punguzeni lugha mbaya ndio maana hatuendelei, acheni kuwa na wivu kurudisha wenzenu nyuma, punguzeni chuki, na lugha za ajabu.

    ReplyDelete
  15. Hivi wadau tuambizane, mwanamke mwenye akili zake timamu, kasoma na kasafiri kiasi hicho, inakuwaje anachukuliwa na mtu mwenye wake wawili na asigundue? Hii imekuzwa au basi ni mpumbavu sana. Ina maana alikuwa anakutana naye wapi? Guest? sasa kama wewe ni mtu wa msimamo mwanamume anakupeleka giuest kila siku, kwake hukujui na wala hufanyi efforts zozote za kumjua unakuwa mtu wa aina gani?

    Nini hasa kikufanye udanganyike hivyo, tamaa au. OK, Tatizo ndo kama hili, unaibuka kutafuta wachumba humu, unaishia kupata wasanii, trust me. Huyu mwamnamke mimi simtaki, ufahamu wake sifuri.
    Nawaone huruma hata waliopeleka barua za kweli, wataambulia shida hapo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...