MWANDISHI WA HABARI MPIGA PICHA WA SIKU NYINGI WA ENZI ZA SHIRIKA LA HABARI TANZANIA (SHIHATA),BONIFACE MASSAGA AMEZIKWA JANA JIONI KATIKA MAKABURI YA NJIRO YA JIJINI ARUSHA NA UMATI WA WANANCHI WA JIJI HILO PAMOJA NA VITONGOJI VYAKE.
MAREHEMU MASSAGA AWALI ALIKUWA MAKAO MAKUU YA SHIHATA JIJINI DAR NA BAADAYE MWAKA 1991 MASSAGA ALIACHA KAZI SHIHATA NA KUAJIRIWA NA KITUO CHA MIKUTANO CHA KIMATAIFA CHA ARUSHA [AICC] KAMA MPIGA PICHA MKUU .

MUNGU AMWEKE MAHALI PEMA
PEPONI MAREHEMU BONIFACE MASSAGA-
AMEEN

PICHA NA NOVATUS MAKUNGA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Patrick L. TsereJuly 21, 2010

    Niliwahi kufanya kazi na marehemu Boniface Massaga nilipokuwa Mkurugenzi Mtendaji wa AICC 2002 hadi 2005. Habari za kifo chake kupitia blog hii zimenisikitisha, hatuna la kufanya zaidi ya kumwombea marehemu Mwenye Mungu Amlaze peponi. Amen. Aidha ninawapa pole zangu na za familia yangu wafiwa na familia ya ndugu yetu Boniface. Ninamuomba Mungu awape moyo wa subira na nguvu ya kuendelea na shughuli za maisha. Bwana alitoa na Bwana amechukua Jina lake lihimidiwe milele.

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 21, 2010

    Poleni sana wanafamilia na wakazi wa AICC Flats Kijenge kwa msiba huu mzito, Mungu awape moyo wa nguvu na subira.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...