Mchezaji maarufu wa kutoka nchini Camerun Eto'o, ambaye kwasasa anachezea timu ya Inter Milan, washindi wa kombe la Ulaya. Jana aliwafurahisha sana wapenzi wa mpira wa hapa Italy kwa upendo wake ndani ya uwanja na nje katika maisha ya kila siku, kama wasemavyo watu wengi ni mtu simpo tu, pamoja na umaarufu wake lakini ni mtu wa watu.
Golikipa wa timu ya Brescia Michele Arcari, alikuwa akihitaji msaada wa kufungwa kamba katika viatu vyake ambavyo vilikuwa vimelegea. Mpira ulikuwa umesimama kidogo kutokana na mchezaji wa Inter kuumia, ndipo golikipa huyo alikuwa anahitaji msaada huo kwa kuwaita wenzake kwenye benchi lake, lakini hawakusikia, alizidi kupiga kelele lakini hawakusikia. Ndipo Eto'o alijitokeza na kumwambia nitakufunga mimi kwani shida ipo wapi. Jamaa hakuamini kama Eto'o kwa umaarufu wake angeweza kufanya hivyo.
Michele Arcari alisema; Eto'o ni mchezaji maarufu sana na ni mchezaji hodari wa hali ya juu, lakini alipiga magoti mbele yangu na kunifunga kamba za viatu vyangu. Nilibaki mdomo wazi (sikuamini kabisa) alisema Arcari, ila pia nafurahi sana maana nilimkatalia magoli mengi kwa kupangua mashuti yake, ila alifanikiwa kunitundika moja, maana timu hizo zilitoka droo 1-1 na mfungaji wa goli hilo alikuwa mwenyewe Eto'o, pia anaongoza kwa magoli ya kufunga katika ligi hii mwaka huu. Ila mengine nilimkatalia kabisa na kufanya timu kubwa kama ya Inter kuto kushinda katika mechi hiyo ya jana. Maana timu ya Brescia ni timu ndogo tu na ukizingatia imepanda daraja la kwanza (Serie A) mwaka huu tu! na inashikiria mkia pamoja na timu yangu ya Cesena, katika msimamo wa Ligi kuu ya hapa Italy - Serie A.
Pia mimi nilicheka sana wiki iliyopita Eto'o alialikwa kwenye TV maarufu, katika kipindi cha watoto, watoto hao walimtwanga maswali mengi magumu, hasa kuhusu rangi yake nyeusi. Aliyajibu mpaka watu walimkubali...mpaka mtoto mmoja alimpenda sana na kumwambia kama Eto'o angeweza kumwoa mama yake mdogo. Eto'o alimjibu tayari nina mke wangu mzuri yule pale mwone, wakamwonesha hapo kwenye TV.
-Eto'o ni mchezaji wa kuigwa kwa Afrika nzima, hasa kwa watu maarufu kama yeye kuto kujivuna na kujikweza pasipo sababu ya kujivuna na kijitambia wao ni wao tu!
Eto'o ni mtu wa watu wasemavyo.
Hongera kwa Eto'o.
www.barakachibiriti.blogspot.com

aaagh shemejiiiiii,ahsante mtoto wa masimba.
ReplyDeleteasli yetu utumwa ati !!
ReplyDeleteEto'o mwenyewe namfagilia kinoma
ReplyDeleteANGEKUWA MWEUSI HUYO ASINGEEENDA ATI.
ReplyDeleteTULITAWALIWA NA WAZUNGU BADO CHEMBE CHEMBE ZIPO ZIPO.
ukitaka kuujua ukweli tafuta mzungu yeyote msimame barabarani halafu itaa we njooo kwa pamoja mwafrika ataenda kwa mzungu kwanza akija kako atakwambia eheee nawe wasemaje.
Yaani aona weye mweusi huna dhamani.