Msanii Diamond akila pozi na kupewa changamoto kutoka kwa Queen wa Pop ambaye alikuwa mshindi wa MTV Award Miaka ya Nyuma Britney Spears mjini London baada ya Urban Tour
Waheshimiwa Wadau Salaam,
Kwa heshima na taadhima URBAN PULSE CREATIVE Inawaomba na kuwasihi watanzania wote pale walipo kuwa wazalendo na kumpigia kura Mtanzania mwenzetu, Ndugu Yetu, rafiki Yetu, Msanii wetu mpendwa Diamond ambaye amebahatika kuwa miongoni mwa wasanii wachache waliochaguliwa kuwania Tuzo za MTV MAMA AFRICA Awards Zitakazo fanyika Nigeria Jijini Lagos Jumamosi hii 11.12.10

Hivyo Basi watanzania na wadau wote wa muziki mnaombwa sana kupiga kura ili Kumwenzesha Diamond ashinde tuzo hii muhimu iweze kuja Tanzania ili kuiwezesha Nchi yetu kujulikana zaidi ulimwenguni na pia kuleta HESHIMA kubwa kwa kila MTANZANIA.

Namna ya kupiga Kura ni kama ifuatavyo:
1. Kwa njia ya simu unaweza kupiga kura yako kwa kuandika neno BNA DIAMOND kisha tuma text kwenda namba 6262, kwa walio nje yaTanzani tuma text 15726.

2. Kutumia Mtandao tembelea tovuti hii http://www.mtvbase.com/splash/mama/

bonyeza mtv mama halafu ingia ndani
ya nominees tunaomba umpigie kura as the best New Act.

Tafadhari fanya sehemu yako pia mwambie na mwenzako.
Asanteni sana Mungu awabariki.

Diamond Platinumz
akishirikiana na
URBAN PULSE CREATIVE

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 21 mpaka sasa

  1. changa la macho hilo ni sanamu ucan see the defference.karibu maddametsaud.

    ReplyDelete
  2. huyu britney anahisi kama diamond ataiba ile tuzo yake,kwa vile alipoiweka mbali

    ReplyDelete
  3. anonymous wa kwanza,
    Hata mie nilijua hilo ni sanamu tu. Duuh wabongo kiboko.

    ReplyDelete
  4. Hivi wewe Frank Iyembe wewe unafanya watu wapuuzi eeeh! Britney wapi si ni msanamu wa pale madametusor! Wacha kuipotosha jamii yote ya nini ni sifa au ushamba. Watanzania ndio maana tunadharaulika hivihivi.

    ReplyDelete
  5. acheni kudanganya watu hiyo ni madame tussauds london ni sanam la britney spears, wabongo tumezidi kudanganyana

    ReplyDelete
  6. Yaani bado tunakasumba ya watu walio enda mamtoni au Ng'ambo au nje ni smart..waliobaki Bongo wote ni washamba..Ni lini tutastarabika..ni yule..aliyestarabika..aliye UK anayedanganya watu kwa sanamu na kujiona yeye zaidi kwa sababu amepanda Pipa..au aliye Bongo huku akiwa mafanikio, amani moyoni na kusoma Blog huku akila supu ya kichwa cha mbuzi au kahawa kwa maanjumati pembeni!!!!!!!

    ReplyDelete
  7. unaujua diamond asingeshika hiyo tuzo ndo ingekuwa kama kweli na sio sanam , lakini aliposhika tuzo ya britney kaharibu , inaonekana kama anamnyanganya, kama wanaigombania tuzo

    ReplyDelete
    Replies
    1. Achen izo la muhimu ni kumpigia kula tu kuweni wazalendo

      Delete
  8. Jamani watanzania tunamatatizo gani? Hivi kunashidagni ya kuandaa CV/profile: Ukiingia kwenye nominees wa MTV utagundua jinsi gani kila mwaka tunashindwa kwa vitu vidogo vidogo. Kwenye profile ya Diamond hamna hata historia yake kama wenzake sijui nani aliyepeleka hiyo profile? Wasanii wote wamepeleka jinsi gani wamehustle kwenye game hadi kuja hapo MTV. Hivi ni nani kweli kwa maelezo haya anaweza kuwa interested na kumjuwa au kumpigia kura Diamond. Tuwe serious na kazi, au hata wewe mwenyewe Diamond ulivyotangazwa ulishindwa kuandaa CV yako umetoka wapi na hupo wapi ili hata kushawishi watu waweze kukupigia kula, kulikuwa na kazi gani kuingiza kuwa wewe ni ambassador wa malaria, umefanya shoo senegal na mtu mkubwa...Let us try to vote but we should count ourselves failure!!!

    ReplyDelete
  9. Mwenzenu mie nilishaingia mkenge nikajua ni picha ya kweli, Isipokuwa nilikuwa najiuliza ni lini Diamond na Britney Spear walikuwa jukwaa moja? yaani ni katika sherehe za nini? Ahsanteni mlioosha macho kwa kunizindua, Ama kweli mjini shule,lakini sio poa hatuna sababu ya kumpandisha chati dogo kisakala namna hiyo. duh!kalagha bhaho na ujinga wako.

    ReplyDelete
  10. Hahahahahah!!!kwanza wangeongea lugha gani?teh teh teh teh sanamu kabisa hiyo!!!dhuuuuuuuuuu

    ReplyDelete
  11. Changa lamacho lenyewe ni hili
    gonga hii link http://www.google.co.uk/images?hl=en&expIds=17259,24472,26428,27147,27213,27744,27868,27886&xhr=t&cp=31&wrapid=tljp1291898804200011&um=1&ie=UTF-8&source=univ&ei=vs8ATbKaFIjqObPW2aYB&sa=X&oi=image_result_group&ct=title&resnum=1&sqi=2&ved=0CC0QsAQwAA&q=britney%20spears%20Madame%20Tussauds%20pics&tbs=isch:1&biw=1245&bih=671

    upuu mtupu huu.

    ReplyDelete
  12. It could be sanamu so tatizo ni nini? Kwani kukutana na britney ni tatizo? mbona kina kiba wanameiba na wanakutana na R kelly, nature kachana live na kina lil kim, I cnt seen any problem . Main issue ni kumpigia kura mtanzania mwenzetu. Tuache kuwa tunakuza vitu vidogo vidogo na kuacha ujumbe wa maana.

    ReplyDelete
  13. ukiingia google na kuandika: ''madame tussauds britney spears wax figure'' hiyo sanamu ya Britney Spears inaibuka.

    Jijini London, maeneo ya Baker street, Marylebone Road London NW1 England, ndani ya Jumba la Madame Tussauds kuna sanamu kibao (wax figures) za watu 'maarufu kwa wazungu' kama Mandela, George Bush jr, Britney n.k

    Hii ni mbaya sana Diamond, bora ungeleta hii picha siku ya April 1.
    Mdau
    Kariakoo
    Mzizima.

    ReplyDelete
  14. tatizo huyu kijana wa mbagara kawa superstar kabla ya kuwa superstar. madoido mengi hadi ukiongea nae unamuonea huruma kwamba unamsumbua.

    ReplyDelete
  15. jamani huyo si britney ni doli lake tu pale uingereza kuna sehemu ya hivyo unalipa pesa kidogo unapiga picha na macelebrity (madoli yao) yanatengenezwa na madame teusand.

    off topic: niliona kutakuwa na misa ya kuombea wafu niliona jina la Mine lakini sikujua kama ni mine yule kaka maarufu au nani.... naomba wadau mnisaidie nimeshtushwa sana.

    ReplyDelete
  16. Wewe Diamond ninataka kupigia kura lakini nimesikiliza clip yako hapa mara tatu kuhusu jinsi ya kupiga kura lakini sijakuelewa bado. Tafadhali anaandika hayo maelezo.

    ReplyDelete
  17. OK HUYU NI BRITNEY LAKINI LINI ALISHINDA MTV AWARD NA DIAMON ALIANZA KUIMBA LINI? NA ALIENDA STATE LINI? MAANA INASHANGAZA,LAKINI LEO HUMU NDANI AFADHALI WAMEMPAKA ALOLETA HABARI NA SIO DIAMOND KWA KUWA YEYE HAJAKUSUDIA HILO,ILA WAACHE USHAMBA WATU WAPO HUKU HUKU UK NA WANAYAJUA HAYO

    ReplyDelete
  18. Haya mimi nishakupigia kura, kila la heri.

    ReplyDelete
  19. OK SAWA NI MADAMTOSADE CHA MUHIMU KAWAOMBA KURA PLS TUMPIGIENI JAMANI LABDA WAMETUDANGANYA ILI WAPATE KULA ZETU SASA SISI TUWAPE HIZO KULA INGAWA TUMESHTUKIA SANAMU LAKINI SIKILIZENI VIDEO YA DIOMOND KATUOMBA JAMANI PLS TUMPIGIE KURA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...