Home
Unlabelled
loliondo kwa babu leo....
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hahaha..yaani huyu haponi maana ameruka foleni..so amevunja masharti mchungaji aliyoyatoa juzi..hapa ni kama anawaonea wengine wasikuwa na uwezo huo
ReplyDeletejamani ina maana wabongo wote wanamaradhi mbona kunatisha? Haya babu dili hilo weka kila kichwa elfu 10.je kuna alopona hizo dawa?
ReplyDeleteKatika Biblia tunasoma pia kuwa Mungu alimfunulia Yakobo (Israel)kuwa watakuja watu toka mbali, wa kila kabila, na kila taifa kukusujudu. Simshangai huyo Babu Mnyakyusa mzaliwa wa Tukuyu Mbeya akifuatwa na watu toka pande zote za nchi Loliondo. Ni ufunuo wa Kibiblia. Ndagaa! Kyala akutulege fijo Mchungaji Ambilikileee!
ReplyDeletemuda sio mrefu tutaona run way imechongwa ili private jet toka mbali ziweze kutua kwa babu na kupata dozzi yake kama kawaida,wewe ukija na ndege,baiskeli,boti,punda,machera uwe na jero tu(Tsh 500)ili uweze pata matibabu yako.kazi ipo loliondo mwaka huu.Mbona hatuoni vingora vya wakubwa au wanakuja kimya kimya?
ReplyDeleteTunakushukuru sana Mzee wetu wa Loliondo kwa kazi unayoifanya cha zaidi tunamshukuru sana Mungu kwa kusikia kilio cha wanadamu na kumtuma mtume wake aitende kazi ya uponyaji. Hatuna cha kukupa zaidi ya asante Mungu wetu. Nasi wanadamu tunatakiwa tupunguze maovu na msujudu Mungu kwa baraka zake kwetu.
ReplyDeleteDah!hii kali amakweli babu kafunika kwa kikombe.Inaonekana hii dawa ni dili, kwani how come watu wanakomaa by any means ili kufika kwa babu.Ila bado naishaangaa serikali kwanini wasifanye utafiti wa kisayansi kujua ni kwavi inatibu.
ReplyDeleteTafadhali nisaidie namna ya kupata helkopta hii. Nipate mawasiliano either na Hans Macha au wenye helkopta yao.
ReplyDeleteYESU ALISEMA ASIYE MGONJWA HAITAJI TABIBU. WEWE ULIYE MZIMA MSHUKURU MUNGU. WAACHE WAGONJWA WAKAPOKEE UPONYAJI. SHETANI HAWEZI KUPONYA. ANAYEPONYA NI MUNGU TU. WANAOBEZA WAKUMBUKE METHALI - USITUKANE WAKUNGA. NA WENGINE WAKASEMA KABLA HUJAFA HUJAUMBIKA. NYINYI MNAOKASHFU OMBENI MUENDELEE KUWA NA AFYA. MUNGU MBARIKI MCHUNGAJI
ReplyDeleteFantastic Hans....treat your Mum, God will always be with you.
ReplyDeleteKILA MWENYE PUMZI YA MUNGU APUMUAYE KWA NEEMA BILA KUWA NA MARADHIO YOYOTE, INAMPASA KUMSHUKURU MUNGU SANA KWA WEMA WAKE KWA SABABU WEWE SI BORA SANA KULIKO WENGINE. NA KILA MWENYE PUMZI YA MUNGU NLAKINI ANAYO MARADHI, BASI INAMPASA KUMUONA TABIBU ALIYELETWA NA MUNGU ILI KUYATIBU MAGONJWA YAKO NA USIPUUZE! TIBA NI KWA AJILI YAKO..
ReplyDeleteMWOMBEENI SANA MTOTO WA HUYU WA MNYONGE (BABU)AMBAYE MUNGU ALIMTOA KATIKA UZAO WA DAUDI ILI AWAONDOLEE WATU SHIDA ZAO P0AMOJA NA MARADHI YAO.
HII DAWA NI KWELI INAPONYESHA MIE MWENYEWE NIMESHUHUDIA>HII NI ZAWADI TOKA KWA MUNGU
ReplyDeleteAnon wa Thur March 17, 09:16:00 AM 2011 - Nakupa hongera sana ujumbe wako ni mzito na mzuri hivyo basi wadau aliye mzima akae kimya atuache wagonjwa lakini kumbukeni shilingi ina pande mbili na hugeuka.
ReplyDeleteJana nilikuwa naongea na daktari hapa Duke University, Marekani, akaniambia kwa vile wanasafari ya kwenda KCMC mwezi ujao itabidi wajiandae kwa ajili ya uchunguzi zaidi. Na mimi nimesisitiza kuwa kuna dawa inaponya magonjwa ya hatari.
ReplyDeleteNiko huku napiga debe kwa ajili ya watu kuja kufanya uchunguzi, unaweza ukakuta Babu anajengewa Loliondo World Hospital in Arusha, Tanzania, East Africa
wewe unaesema wameruka mstari nani kakwambia hapo wanatua sasa unataka watue kwenye foleni. Watu wengine mtumie akili kabla ya ku comment kwanza inatua eneo la wazi then wanaenda kupanga foleni kama wengine walivyopanga akitua penye watu panga likiwakata je? Common sense is not common to everybody
ReplyDeleteWATU WALIOKUNYWA DAWA YA BABU NA KUPONA WAJITOKEZE KUTOA UKWELI KWANI MPAKA SASA NI MAELFU WALIOKUNYWA ILA MAJIBU NI MACHACHE,KWANI KUNA WASIO NA IMANI ILI WAWEZEKUAMINI NA PUPATA MSAADA HUO.KUNA FISADI MMOJA ROSTAM AZIZ ANADAI HIYO DAWA SIO YA KWELI HEBU JITOKEZENI ILI AWAJIBIKE NA KUJIUZURU UBUNGE KWA HILI FISADI TUMELICHOKA NA LINATAKA KUWADANGANYA WATU ILI WASIPONE.
ReplyDeleteMDAU
Haya bwana Macha, Inaonekana ni wachagga tu watakaoweza kupata huduma kwanza.
ReplyDeletesalaleeeeeee duh mpaka helikopta duh ila babu anatibu asikwambie mtu ndg yangu looooooooo
ReplyDeleteKwanza kabisa ndg watanzania wenzangu tumshukuru mungu kwa muuijza huu aliotuletea huyu mpendwa wetu babu asante mungu. napemda kusema machache kuhusu mchungaji mwingira na kakobe wake nyie ni wezi mbele ya watu na mungu mnawaibia waumini wenu kwa kuchukua mishahara yao vitu vyao kwa faida zenu wenyewe.
ReplyDeletehuo ni wivu nyie hamna mpya ni wadanganyifu tu tumewashtukia hatuji tena kwenye makanisa yenu igeni mfano wa babu pesa kidogo matibabu makubwa. Ndg wananchi wenzangu msiwasikilize kakobe na mwingira hawa ni matapeli tu wa kutupwa. asante babu
kudadeki....
ReplyDeleteHivi jamani hebu niambieni ,kweli kuna mtu anaweza thibitisha na kutoa ushuhudaa???? kwamba .....kuna mtu ambaye ni HIV positive,nikimaanaisha vipimo vya hospitali vimeonyesha then kaenda kwa Ambilikile a.k.a Bubu kupata kikombe....baada ya siku kadhaa kaenda kupima na hospitali na akawa Negative????
ReplyDeleteingelikuwa vizuri sana kama babu ange shirikiana na serekali kuchkua takwimu ya maradhi waliyokuwa nayo watu. si lazima waweke wazi maradhi gani japo kwa namba tu. kumbe watanzania ni rahisi kupigwa limbwata. kiasi tutulie kwa kila baya tunalofanyiwa....tumeshakata tamaaa sasa wacha tunywe hayo maji ya "bwana" tuzidi kutulia.
ReplyDeletejamani naombeni msaaada kokudi helikopta bei gani??nataka kumkodishia mama yangu..
ReplyDeletehuyo annon hapo juu vipi??eti ni wachagga tuu wataokaoweza kupata huduma,kwani babu anatibu wachagga pekeyake..acha ujinga wewe
ReplyDeleteHIVI NYIE MNAOJIFANYA MNAJUA DINI...WEWE UNAWEZA KUAMINI HUYU NI NABII/MTUME.
ReplyDeleteNDIO MAANA TANZANIA WATU WANANUNUA VIUNGO VYA BINADAMU WAKITEGEMEA KUPONA AU KUPATA UTAJIRI...SHAME ON YOU!!! HUYO NI MGANGA SIO NABII/MTUME KAMA ANAVYODAI..FUNGUA BIBILIA AU KURANI UTAJUA MAANA YA MTUME NA MTUME WA MWISHO DUNIANI. HIVI VITABU VINAZUNGUMZIA WATU WATAOJIDAI NI MITUME NK. MTUME ATAYEREJEA KABLA YA KIAMA NI YESU (NABI ISA) HAKUNA NABI MWINGINE
WADANGANYIKA....
ReplyDeleteNilikuwepo alikuwa jamaa toka Kenya. Watu tunapona. Mimi nilikuwa na sukari kwa zaidi ya miaka 10 na cliniki yangu ilikuwa kwa Dr Abbas Kariakoo. Nimekunywa dawa jumanne tarehe 15.03.2011 na mpaka leo sijanywa dawa yoyote na nimepima sukari baada ya kula na kunywa nikakuta 9.9 mm/dl. Nawashauri wanaopuuza tiba hii waache maana sisi tuliokuwa wagonjwa tunamwomba MUNGU awape watu hawa moja ya magonjwa haya ili wajue ni nini kuwa na ugonjwa usio na tiba wala kinga. Naomba waliopona wajitokeze kutoa ushahidi ili wanaodhihaki tiba hii waaibike.
ReplyDeleteJami mimi bado ni tomaso...Aliyepona aje atuambie...Na si kupona BP, Malaria au kisukari...Nataka nione aliyekua HIV+ na sasa ni HIV-...
ReplyDeleteHalafu huyu baba ni myakyusa ilikuaje aende huko Loliondo...Au ndio mizizi ipo huko?
Watu waambiane ukweli kuliko kupoteza hela hivi kwenda huko...
na babu hajatoa neno kuhusu jinsi ya hela ya usafiri wa huko? hiyo hela ikipatikana kwa ufisadi mtu anapona au la? Watu wataiba mahela manake najua hela ya kwenda kuhiji ni lazima uipate kihalali la sivyo utakiona ukienda huko...
Shuhuda nyingi tumeziskia na aliye na imani na babu na aende hazuiwi kama anapata kibali toka kwa mungu wake.na tusipende kuhoji haya kama unaumwa kimya kimya inuka kapate kikombe.ila cha muhimu mwamini mungu zaidi kuliko mwanadamu.mungu wetu ni mungu mwenye wivu.amtegemeaye mwana huyo amelaaniwa maandiko yanasema.so msifu na kumtukuza mungu kwa atakachokukirimia.
ReplyDeleteHII NI SHIRK KUBWA. JAMANI WATANZANIA ZINDUKENI. SHIRK NI MBAYA
ReplyDeletendio hiyo ni shirki kubwa.yeye kama kweli anatibu kwa nini asiruhusu wasiojiweza wapelekewe dawa?analazima akupe palepale dawa unywe?asikudanganye mtu,dawa ni qur'an peke yake.
ReplyDeletebabu kweli yuko juu. Mungu baba namshukru kwa kazi aliyompa BABU NAKUOMBEA UZIDI KUWA NA NGUVU ZA KUHUDUMIA WATU WA MUNGU.
ReplyDeletehuyo babu ni muongo na maji yake machafu wewe fikilia ukiumwa homa ukwanya dozi kamili utapona hata usipoamini huyo mjinga anaweka imani mbele ili asirudiwe kudaiwa na wagonjwa wasiopona na anasema mungu kamuotesha. Mungu hatibu kwa mzizi Mungu hutibu kwa Neno.? na sirikari ya tanzania lina angaria huyo fisadi mganga anataperi watu au viongozi wa chama cha majambazi. ccm wamo
ReplyDeleteWapendwa watu wa Tanzania sasa actually watu wasio na uwezo na wenye uwezo watibiwa na kupona kila siku. Je mnahitaji shuhuda nyingi kiasi gani ili muamini? Mtu anapoenda kupata dawa anaomba Mungu apone sio ili akufurahishe ili uamini kutokuamini kwako. Kwa wale waliopata ujasiri wa kutoa shuhuda zao it is a blessing lakini nafikiri kabisa jiwekeni katika position ya mgonjwa hata tu kwa sekunde chache, mtu anaomba Mungu amponye awe mzima. ukibahatika kushiriki furaha yake jinsi alivyopona ni vizuri lakini kama ameamua kumrudishia tu Mungu wake utukufu pia it is ok. Wewe kama huumwi usiwakataze na kudiscourage wenzako wasiende kwa babu ina maana unapenda wao waendelee kuteseka na kuumwa? Naamini unapenda wapone waache wakapone basi. Asanteni.
ReplyDeletetusubiri after kama miezi sita kama hamjaona watu wamekua machizi. kwani hospitali ni za nini if this is the case wazifunge na watu wawe refered to babu. wake up tanzanians tunarudi kwenye ujima
ReplyDeleteMungu na ashukuriwe kwa kuwatendea waja wake muujiza..... amini na utapona.
ReplyDeleteJAMANI NIMESIKIA ETI BABU KAGEUKA NYOKA NA KAKIMBILIA POLINI HABARI ZIMEZAGAA HUKU KENYA...VIPI ZINA UKWELI?
ReplyDeleteNilienda kwa babu na mume wangu mwezi wa julai lakini sukari bado inatusumbua labda kama dawa hiyo inachukua muda mrefu kufanya kazi mwilini. Asante
ReplyDeleteMukumbwa