Marehemu Mama Asha Nasibu
Shefa enzi za uhai wake

MAMA YETU MPENDA MAMA ASHA NASIB SHEFA( DA ASHA) AMEFARIKI DUNIA USIKU WA KUAMKIA LEO JUMATATU TAREHE 7 MARCH HOSPITALINI AGAKHAN JIJINI DAR BAADA YA KUUGUA KWA MUDA MREFU.

MAZISHI YATAFANYIKA HUKO TANGA KESHO JUMANNE TAREHE 8 MARCH BAADA YA SWALA YA DHUHRI. Marehemu ameacha watoto watano na mume na maisha yake yote alikuwa mtumishi katika idara ya mapato (TRA). MUNGU AMUWEKE MAHALI PEMA

- AMIN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. Poleni sana ndugu na jamaa wa karibu na hata watu wote mlioguswa na msiba huu. Tumwombe mungu atupe nguvu katika kipindi hiki cha kuondekewa na mpendwa wetu, bila kusahau yote ni mapenzi yake aliyetuumba. Pole sana Rafiki yangu mpenzi Fatma. Salaam kutoka UK kwa rafiki yako mpenzi.

    ReplyDelete
  2. Polen sana wapenzi wangu Viwe na fatu na wote mnaoguswa na msiba huu mungu atawapa nguvu na subira. Mungu katupa na katwaa Mungu amuweke mahala pema Amin
    Mdau Stockholm

    ReplyDelete
  3. Mungu amuweke mahali pema kwa kweli huyu dada alikuwa mtu mzuri kupita maelezo. Tulimpenda lakini mungu kampenda zaidi.
    Mdau TRA

    ReplyDelete
  4. Ina lillahi wainna ilaihi rajiuun. Pole sana fatuma na wafiwa wote, inahitaji subura ya hali ya juu. Twamuombea dua anakokwenda kuwe ni bora zaidi ya alikotoka, amini.
    Wajina lako, Washington DC.

    ReplyDelete
  5. Inna Lillahi Wainna Ilaihi Rajiuun.
    Words cannot heal the pain of losing someone so dear. Our mom will always remain close to our heart because she left behind beautiful memories for us to cherish. May God give us the strength to overcome the pain. AMEN

    ReplyDelete
  6. Poleni sana Viwe na wadogo zako, inshallah Mungu atakupeni moyo wa subira na uvumilivu, dua zetu ndio zawadi kubwa kwa marehemu tuko pamoja na nyie katika kuomboleza msiba huu, Mungu atamjaalia mapumziko mazuri huko aendako. Amin.
    Stockholm.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...