Kamati ya Bunge Huduma za Jamii leo imefanya ziara katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kutembelea Kitengo cha  Tiba ya Figo ili kufahamu hali halisi ya utuoaji wa huduma za tiba ya figo hususani uchujaji wa damu.  

Kitengo hiki kinatoa huduma kwa wagonjwa waliolazwa hospitalini na wagonjwa wa nje kwa kuhudumia na kusimamia wagonjwa wenye magonjwa ya figo waliolazwa kwenye jengo la Mwaisela na walio kwenye idara zingine kwa kushiriki matibabu yao. 

Kitengo kinaendesha kliniki kwa wagonjwa wa nje, mara tatu kwa wiki, zikiwemo za kufuatilia maendeleo ya wagonjwa waliowekewa figo nyingine; waliojitolea figo kwa jamaa zao; na wenye matatizo mengine yote ya figo kwa ujumla. 

Aidha kitengo hiki hutoa huduma ya uchujaji wa damu (dialysis) kwa wagonjwa ambao figo zao zimepoteza uwezo wake wa kufanya kazi. Kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, kitengo kinamwandaa mgonjwa wa figo na aliyejitolea kumpa mgonjwa figo kwa matibabu na kitengo hiki kinasimamia uchunguzi wa magonjwa ya figo kwa kushirikiana na Maabara Kuu ya Hospitali ya Taifa Muhimbili. 

Kitengo hiki kilizinduliwa rasmi na Mh. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Novemba 2, 2009. Kitengo kina jumla ya madaktari bingwa wawili wa tiba ya magonjwa ya figo, madaktari waandamizi wanne na wauguzi tisa. Ifuatayo ni habari katika picha kuhusiana na ziara ya Kamati ya Bunge Huduma za Jamii.
DSC03842.JPG
Baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma za Jamii wakipata maelezo toka kwa Dkt. Linda Ezekiel, Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Figo  (hayupo pichani).
DSC03847.JPG
Waliosimama kutoka kushoto ni Dkt. Hedwiga Swai Kaimu Mkurugenzi wa Tiba, akifuatiwa na Dkt. Linda Ezekiel, Bw.Makwaia Makani ambaye ni Mkurugenzi wa Utumishi na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela kwa pamoja wakisikiliza maelezo ya huduma ya figo toka kwa Dkt. Linda
DSC03856.JPG
Dkt. Linda Ezekiel (kushoto) akitoa maelekezo kwa  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma za  Jamii  Mh. Margaret Sitta pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela wakimsikiliza Dkt. Linda kuhusiana na huduma ya kuondoa sumu mwilini kwa kutumia mashine maalumu (figo mbadala/artificial kidney).
DSC03862.JPG
 Aliyekaa kitandani ni mdau wa huduma ya figo akiwasikiliza wajumbe wa kamati ya Kudumu ya Bunge Huduma za Jamii
DSC03864.JPG
  Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge, Huduma za  Jamii  Mh. Margaret Sitta pamoja na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dkt. Marina Njelekela wakimsikiliza Dkt. Linda kuhusiana na huduma ya kuondoa sumu mwilini kwa kutumia mashine maalumu (figo mbadala/artificial kidney).

DSC03869.JPG
Wajumbe wa Kamati wakifuatilia kwa umakini kabisa maelezo ya huduma za figo kutoka kwa Dkt. LindaDSC03875.JPG
Mmoja na wadau ya huduma za figo akifafanua jinsi alivyopata huduma kwa wajumbe wa Kamati ya Bunge. 
DSC03888.JPG
Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili Dkt. Marina Njelekela akimsikiliza kwa makini Mjumbe wa Kamati ya Bunge ya Kudumu, Huduma za Jamii, Mh. Matha Mlata
DSC03894.JPG
Dkt. Njelekela akiteta jambo na Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu, Huduma za Jamii Dkt. Faustine Ndugulile na Mjumbe wa Kamati hiyo Dkt. Maua Daftari

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Giza tupu
    Ndugu washa taa tuone hizo picha

    ReplyDelete
  2. mdau umesema kweli. au tanesco nao wako huko?

    ReplyDelete
  3. Naona huyu ripota wa Muhimbili bado hajaset camera yake sawa kudownload kwenye hii libeneke. Nakumbuka ripoti yake ya wiki chache nyuma mambo yalikuwa hivi hivi. Giza tupu!!!

    ReplyDelete
  4. Dr. Linda Ezekiel tunampa hongera kwa kazi hiyo ya kuwahudumia wagonjwa wa figo ila aache tabia yake ya kugombeza wagonjwa na kuwatishia tutowasaidia waweze kwenda kutibiwa. Ana tabia ya majivuno sana huyo daktari, aache maramoja hiyo tabia sio nzuri. Yeye kama mkuu wa Kitengo aelewe kuwa wagonjwa wake ndio hao sio kwamba walipenda kuugua anavyoringa na kauli zake za hovyo sio jambo zuri. tunamtakia kila la kheri

    ReplyDelete
  5. Ewe ripota wa Muhimbili
    Watufanya tumlalamikie TENESCO kwa giza bure, naona makosa yapo kwako. Nafikiri hutumii common Digital photo formats,niruhusu nikukumbushe kuwa common formats are:
    1.JPEG,yaani Joint Photo Expert Group
    2.TIF
    3.GIF
    4.PNG
    Tafuta software na kuchange picha zako to JPEG kabla hujamtumia Mjomba
    Wakatabahu

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...