Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 24 mpaka sasa

  1. Popobawa mzee wa majunguFebruary 07, 2012

    mtajua wenyewe! kwanza mimi nipo safarini. hata hivyo shangazi dada yake bibi yule wifi yake mkewangu si anaweza kwenda kuchekiwa malaria India.kwa taharifa yenu kinachoniumiza kichwa saizi ni kurudisha mtaji niliotumia kupata nafasi ya Ubunge na mambo ya Uchaguzi wa 2015.
    asanteni.
    wenu katika kuendelea kulimega taifa kwa nafasi ya kujidai
    Kiongozi wenu!( tena mlie nichagua wenyewe).

    ReplyDelete
  2. Yaani blog ya jamii leo mmenivunja mbavu..Nilishtuka kidogo nilipoona Tangazo sikusoma hata kichwa cha habari.nikadhani ni Muhimbili.Serikali toeni Maamuzi Magumu sasa

    David V

    ReplyDelete
  3. Duh kumbe makelele yangu ya matumizi sahihi ya kiswahili yatachukuwa muda kuwafikia wananchi. Madaktari wazima wanaandika neni "dharula" badala ya "dharura" ipo kazi

    ReplyDelete
  4. hili tangazo lingewekwa pale muhimbili ndo serikali ingeshtuka!

    ReplyDelete
  5. Kaka Michuzi, hivi nani wanamshauri JK?

    Kikwete na rais mzuri sana na mwenye uvumilivu, na asiesahau fadhila. Lakini haya ndio now yanakuwa yeye ni tatizo. Uhuru wa vyombo vya habari na wanachi kuongea kama hivi, Mkapa asingeweza kuruhusu.

    1. Kwani vikao vya kujadili posho, kumwapisha balozi, visingeweza kusubiri kwanza mpaka amalizane na wauguzi ndio haya mengine yafuate bkoz watu wanakufa.
    2. Ingekuwa naweza mshauri rais, ningemwabia ktk hotuba yake asiongelee swala la madaktari kwani pinda alisha ongelea, na wakishamilizana na madaktari, serikali iwaamuru madaktri kupitia mwakilishi wao ndio aongee na waandishi wa habari kuwa mgogoro umeisha. Kama kuna mapungufu yaliotokea ktk mgogoro huu serikali, serikali ishughulikie kimya kimya.
    3. Failure kumaliza mgogoro mapema, inapandisha wanachi hasira na inaleta picha kuwa hamjali wananchi kwakua mnatibiwa nje au kupitia bima za afya ambazo masikini hawana.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  6. Hata nyie wauguzi kuna wanafiki miongoni mwenu, kugoma ni haki yenu ya kikatiba, lakini mkiamua kugoma au kusema jambo basi limaanishe wote, sio wengine wa mikoa fulani au hosipitali fulani wanagoma na wengine mnaendelea na kazi. Kwani katka majadiliano yenu na serikali ikatokea serikali ikaongeza japo sh 10/= ktk madai yenu, watakao faidika ni wale tu waliokuwapo katka mgomo au hata wale ambao waliokuwa wanajirudisha nyuma kujifanya hawataki kile kinacho daiwa na waliogoma? Umoja ni nguvu, mgomo ukiisha jisafisheni muwe kitu kimoja sio wa sura mbili

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  7. lakini habari imefika. sio uchambuzi wa kisw hapa

    ReplyDelete
  8. We anonymous wa Tue Feb 07, 11:44:00 PM 2012- Nakubalina na weye, lakini si Rais tu, bali viongozi na raia wote inabidi wawajibike. Kwa mfano, uzembe wa mabomu kulipuka ovyo,Umeme usioeleweka,Meli kuzama-Nungwi, watu kupigwa katika maandamano ya Arusha na maskando mengine kibao, sijasikia kiongozi hata mmoja kujiuzulu au kufukuzwa kazi. Madaktali lazima wagome mpaka kieleweke, wapewe haki yao.(ndiyo nasema labda kwa vile hatuumwi kwa sasa au hatuna ndugu anayeumwa, lakini wote kuna wakati tumepita au tunapitia hospitali. Mpaka kila mtu atakapoanza kuwajibika,kutowapigia kura viongozi wabovu ndiyo bongo itakapoanza kusonga mbele.

    ReplyDelete
  9. Kudadadadadadadddadeki......! Nyerere alishajifia siku nyingi. Sasa hivi mwenye panga kali ndiye anayekata pakubwa. Watanzania kazi yenu ni kulipa kodo tu...... Serikali itawasaidia namna ya kuzitumia. Waganga wa kienyeji changamkieni biashara msije kufa malofa. Kina mama na watoto mtajiju, wenzenu wakipiga chafya tu wanaenda India. Kudadadadadadadadadadadadeki! Na bado. Si mliwachagua wenyewe? Huko tunakokwenda itakuwa kama Syria.

    ReplyDelete
  10. Wewe unayekosoa kiswahili umeona ulivyoandika 'neni' badala ya 'neno'?Mtu yeyote anaweza kufanya Makosa ndugu yangu.

    David V

    ReplyDelete
  11. Naomba kuwakilisha hili na naomba watanzania wote tulitambue, Upumbavu na Ujuha upo kwa wananchi na si viongozi. Sisi ndio tuliowachagua hao kwahiari zetu pasi ya kusurutishwa na mtu. Tulihitaji viongozi waliojali matumbo na mifuko yetu nyakati za chaguzi bila kuhoji utendaji na uwajibikaji wao. Siku zote wananchi ndio wanaoleta maendeleo na umaskini wa Taifa kupitia maamuzi yao, Kama uliamua kumchagua asiyekujali na asiye na sifa ya kuongoza ni vipi utegemee kuongozwa. Wapo tuliowachagua kwa kuwa walikuwa wasanii mashuhuri, wapo waliokuwa waandishi waliofahamika, wapo waliokuwa waganga wa kienyeji, wapo tuliowachagua kwa utajiri wao, wapo tuliowachagua sababu wazazi au ndugu zao walituongoza nyakati za nyuma hii yote tukitegemea kuwa na maisha mazuri sababu ya umaarufu wao. MAENDELEO HULETWA KWA UTENDAJI NA UWAJIBIKAJI NA SI UMAARUFU. Kamwe sitokuja kuhangaika kuongoza taifa hili hata kwa ukatibu kata mpaka pale tutakapotambua umuhimu wetu katika maendeleo kama wananchi..

    Kijana Mdogo

    ReplyDelete
  12. NAOMBA KUULIZA BUGANDO NI YA SERIKALI AU YA KANISA KATORIKI?

    ReplyDelete
  13. hivi mpaka taarifa za misiba kila kona zisikike ndo watawajibika??

    ReplyDelete
  14. kwahio wooote hamkuona materrorrists wapya aka madaktari ambao wametutekanyara na wanadai ransom, tofauti yao na wale wanaojizungusha mabomu na kutekanyara ndege ni nini???

    ReplyDelete
  15. Hivi nchi hii in uongozi jamani? hata kama wanatatua kimya kimya basi tuone ufumbuzi wa Tatizo, mbona srikali na madaktari mnatuwekeka sisi wananchi na hasa wategemezi wa huduma mtu kati?
    hivi kweli ndugu zangu fadhila ya kura zetu ndio tulie namna hii
    Jamani tunawaomba mlioko madarakani hebu sikilizenu vilio vya wagojwa, hebu jifikilieni kama ingekuwa wewe ungeweza kuvumilia, serikali hamumkomoi daktari, hebu ombeni busara kutatua jambo hili, kuweni wajinga wa leo waelevu wa milele, acheni mivutano isiyo na tija kwa watanzania jamani,
    waheshimiwa tusisibiri kusujudiwa kwani sisi sio mungu, tuwaite wahusika tuzungumze, watu wanakufa kwa kukosa huduma, mtaenda kujibu nini kwa mwenyezi mungu??

    ReplyDelete
  16. kibanga msese wengine hawagomi kwa sababu za kiimani, mtu kama anaona dhambi kuacha binadamu mwenzie afe huku anaona, si rahisi akagoma, hakuna sababu ya kuwalaumu madaktari ambao wanaendelea na kazi huku wengine wamegoma, alieamua kugoma agome asietaka kugoma nae sawa tu hakuna lawama

    ReplyDelete
  17. Stupid people......really??kwahyo kugoma kwao wanawakomesha serikali ama sisi??OMG sometimes najuta hata kwann mm ni Mtanzania,nchi haina mwelekeo kabsaa....hawa madaktari waone aibu kwakweli!!!!

    ReplyDelete
  18. We Anonymous wa Wed Feb 08, 04:30 AM 2012 unajua kulipuka kwa mabomu ni uzembe wa nani? Isitoshe katika historia ya kulipuka mabomu siyo mara ya kwanza duniani. Tafuta sababu halafu ndiyo ulaumu kama jinsi watu wanavyoilaumu serikali katika mgomo wa madaktari.

    ReplyDelete
  19. Hili tangazo linaonyesha kuwa watu wamechoka sana na utendaji mbovu wa baadhi ya viongozi wa serikali. Kwa kweli viongozi wakuu wa Wizara ya Afya ndio waliolikoroga hili kuachia kutatua matatizo yakingali mabichi wameyaachia hadi kufika ngazi ya taifa na mgomo kuwa sugu. Ni dharau ya viongozi wakuu wa Wizara ya Afya iliyotufikisha hapa. Hivi walishindwaje kuyatatua matatizo haya tangu awali?

    ReplyDelete
  20. Nyerere alishasema, kuwa "Ikulu si mahala pa kukimbilia", ndio haya sasa katibu mkuu na waziri wanachemka kushughulikia hili na ni wiki ya pili sasa, ilitakiwa sasa Raisi ndio aingiie kati, maana wateule wake wameshindwa kufanya kazi.

    ReplyDelete
  21. Jamani tujali maisha yetu na wananchi kwa ujumla, halafu pesa baadae. Tuige mifano ya wenzetu

    ReplyDelete
  22. Tatizo la viongozi wa Africa hudhani kuwa, kwa wao kuchaguliwa kuwa viongozi basi wana akili sana na wanajua zaidi kuliko mtu yeyote wanae mwongoza, hili ni sahihi hasa wanaposifiwa na wapambe au washauri wao kwa mambo ya kuwapendeza tu.

    Madaktari kama wameamua kugoma au kuto goma basi inabidi iwe kwa wote, na sio nusu nusu, kwani hata wao walioamua kuendelea na kazi nao wamechemka kuendelea kwakuwa overloaded. Ni jukumu la idara husika kufuatilia na kutatua matatizo sio tu ya wauguzi, ili yasifike hatua iliopo.

    Madaktari sio terrorist, kwani walileta matakwa yao, hayakusikilizwa wafanyaje? Kuna mbunge au waziri ambaye mshahara wake haujatoka kwa kipindi cha miezi mitano?

    Wtanzania, tusilalamikie matokeo, lazima tujikite kujua chanzo cha matatizo. Tusilalamikie mgomo wa madaktari, tulalamikie chanzo cha mgomo ili kesho yasitokee.

    Kibanga Msese

    ReplyDelete
  23. HATA MKIGOMA TUTA PATA HUDUMA YA SHILINGI 500 KWA BABU. KWANZA DAWA ZENU HAZITUBU KUNA DAWA YA BABU WA LOLIONDO INATIBU VIZURI SANA. ENDELEEENI KUGOMA HATUWAHITAJI SASA HIVI.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...