Tarehe 11/07/2012 Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama iliwasilli nchini Uingereza kwa ziara ya kikazi. Kamati hiyo uliyongozwa na Mwenyekiti wake Waziri Mkuu mstaafu, Mhe. Edward Lowassa aliyefuatana na wajumbe wengine ambao ni Mhe. Beatrice Shelukindo,Mhe. Rachel Mashishanga, Mhe. Vita Kawawa, Mhe. Khalifa M. Khalifa na Bw. Ramadhani Issa Abdalla ambaye ni Katibu wa msafara.
Tarehe 12/07/2012, kamati ilitembelea bunge la Uingereza na kupata uzoefu wa namna bunge hilo linavyoendesha shughuli zake. Aidha Kamati ilitembelea nyumba na mali zinazomilikiwa na serikali ya Tanzania nchini Uingereza.
Leo tarehe 13/07/2012 kamati ilitembelea ofisi ya Ubalozi na kuzungumza na Maafisa wa Ubalozi. Kupitia mazungumzo hayo, Kamati ilifanikiwa kusikia shughuli za ubalozi, mafanikio na changamoto mbalimbali zilizopo katika utekelezaji wa sera ya Diplomasia ya Uchumi nchini Uingereza. Aidha Kamati ilipata nafasi ya kutembelea taasisi maarufu inayojishughulisha na masuala ya sera za kimataifa ya CHATAM HOUSE na kuelezea sera za Tanzania katika masuala ya siasa za kimataifa na uchumi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mbunge wa Monduli na ambaye ni Mwenyekiti wa
Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Mh. Edward
Lowassa(nne kushoto), Balozi wa Tanzania nchini Uingereza, Mh. Peter
Kallaghe(tano kushoto), wakiwa pamoja na wajumbe wa Kamati ya Bunge.
Kutoka kushoto , Mh. Rachel Mashishanga, Mh. Beatrice Sherukindo, Mh.
Vita Kawawa, Mh. Khalifa M Khalifa(tatu kushoto), Naibu Balozi, Mh.
Chabaka Kilumanga na Katibu wa Msafara
Pichani, Mheshimiwa, Edward Lowassa (Waziri Mkuu Mstaafu), akiwa katika picha ya pamoja na Balozi, Wajumbe wa Kamati na Maofisa wa Ubalozi.
Waziri Mkuu Mstaafu, Mheshimiwa Edward Lowassa akisindikizwa na Mheshimiwa Balozi Peter Kallaghe na Maofisa wa Ubalozi baada ya kumaliza mkutano na Maofisa wa Ubalozi. Picha na Allly Rashid Dilunga
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...