Msanii wa muziki Judith Wambura maarufu kama Lady Jay Dee akiwa
ameshikwa mikono kusaidiwa kushuka kutoka mlima Kilimanjaro aliko
panda Jaanuary 8 mwaka huu na mumewe Gadner G Habash kwa lengo la
kutangaza utalii wa ndani.
Mhifadhi mkuu wa mlima Kilimanjaro Erastus Lufungulo akimuongoza
msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka mlima
Kilimanjaro,shoto mwa Jay dee ni mpiga picha wa JayDee,Bw Justine Bayo.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi cheti cha
uthibitisho wa kufika kileleni msanii Lady Jay Dee.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akimkabidhi Gadner Habash
cheti cha uthibitisho wa kufika kileleni Gadner G Habash.
Mhifadhi mkuu wa hifadhi ya mlima Kilimanjaro (KINAPA), Erastus
Lufungulo akimkabidhi cheti Bw. Justin Bayo baada ya
kufanikiwa kufika katika kilele cha Uhuru.
Msanii Lady Jay Dee,mumewe Gadner na mpiga picha wao Justine
wakimsikiliza kwa makini mhifadhi mkuu wa Mlima Kilimanjaro Erastus
Lufunguro(hayupo pichani).
Mume wa msanii Lady Jay Dee aliyekuwa ameambatana nae katika safari
hiyo ya siku tano Gadner G Habash akizungumza na waandishi wa
habari (hawako pichani) mara baada ya kushuka katika lango kuu la
Marangu.
Msanii Lady Jay dee akizungumza na wanahabari( hawapo pichani) mara
baada ya kufanikiwa kushuka salama kutoka mlima Kilimanjaro.
Mhifadhi mkuu (KINAPA)Erastus Lufungulo akizungumza wakati wa hafla
fupi ya kumpoekea msanii Lady Jay Dee mara baada ya kushuka kutoka
mlima Kilimanjaro.
HONGERA JD TUPE PICHA AKIWA KILELENI .
ReplyDeleteHONGERA LADY JD na mumeo.tupeni picha mkiwa kileleni
ReplyDeleteHongera komando Jide
ReplyDeletesasa kama huyo ndo mpiga picha wao nani alikuwa anapiga picha?
ReplyDeletemkuu wa wilaya ya nanihii, mbona haujaweka picha za kuonyesha wamefika kileleni mwa mlima?
ReplyDelete