Kaka Michuzi msaada kwenye tuta,
Naomba uniwekee tangazo hili kwenye blog yako mdogo wangu kapotea hajulikani alipo.
Mwenye picha hizi ni mkazi wa mpanda na aliondoka nyumbani tarehe 7/03/2013 toka tarehe aliyoondoka hajarudi na hajulikani alipo.
Tunaomba kwa yeyote atakayemwona mahali popote atoe taarifa polisi au atujulishe kwa namba zifuatazo:
0764 456 619/ 0659 556 965/0756 093680.
Sawa Tangazo limetufikia,
ReplyDeleteTutafanya jitihada kumsaka.
Jambo la ziada kwetu wote ni kuwa ktk rika la huyu kijana ndio muda ambao mtu anakuwa na changamoto sana hasa akifikiri maisha yake ya baadae, hivyo anatakiwa (i)apewe ushirikiano mzuri,(ii)apewe mwongozo sahihi na kupewa utulivu wa Kisaikolojia (iii)apewe moyo na sio kukatishwa tamaa vitu ambavyo mara nyingi humsababishia kijana awe anachanganyikiwa na asijue la kufanya.
Wakati mwingine baada ya mikanganyiko na mazingira anayopewa nyumbani yasiyo na mwelekeo huo (i),(ii) na (iii), anaweza kuamua kutoweka na kutafuta ustaarabu wake wa maisha huko anakokujua.
Hana jina????Umri gani?? Hali yake ya akili/ubongo?? Hana alama za mwili? Hana hata historia ndogo tu ya maisha???? Too many obvious questions ...
ReplyDeleteKama hutaki vijulikane, kuna haja gani ya kutangaza???
Bwana kaka, inaonyesha mmembugudhi Bwana mdogo Kisaikolojia ndio maana akaakumua kwa ghadhabu kuondoka nyumbani tena bila taarifa!
ReplyDeleteMaisha ya ubepari ktk zama hizi yametuathiri sana.
ReplyDeleteUkiwa ktk baadhi ya Ukoo kama unaonekana huchangii kitu, labda kipato huna kwa kipindi hiki, kwa kweli inabidi uwe na moyo kwa kuwa makubwa yatakukuta!
Usishangae kuitwa mvivu!
Usishangae kuitwa huna akili!
Usishangae kuitwa goigoi!
Jamani maisha yanaweza kukataa hamjui?, halafu baadae yakafunguka?
Sasa ukishindwa kuvumilia kwa kejeli hizo hapo juu kutoka kwa ndugu na jamaa, ndio unaweza kupata ujasiri wa kusema potelea mbali lolote na liwe wacha niondoke niende kusikojulikana!
Wadau wa 1 wa 3 na wa 4 kwa kweli maisha yanahitaji sana ushirikiano na walio karibu yako.
ReplyDeleteMara zote kubomolewa Kisaikolojia ndio mwanzo na huchangia sana maamuzi magumu na mabaya mtu kufanya!
Ndio maana unaweza kukuta penye mfarakano mtu akikosa ushirikiano mzuri na ushauri akafanya mambo mabaya sana ikiwezekana akauwa!
Hivyo wandugu tuwe na utamaduni wa kujengana Kisaikolojia hasa ktk vipindi vigumu kimaisha na sio kubomoana.