Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL unawatangazia abiria wote na wananchi kwa jumla  kuwa kutokana na sababu za kiufundi unasikitika kuwa treni ya abiria iliyopangwa kuondoka leo Ijumaa Machi 15, 2013 saa 8:30 mchana  imeahirishwa  hadi kesho Jumamosi  Machi 16, 2013, saa 8:30 mchana.

Tafadhali atakayesikia tangazo hili amuarifu na mwenzake.
Uongozi wa TRL unaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza..

Imetolewa na Ofisi ya Uhusiano kwa niaba ya Kaimu Mkurugenzi Mtendaji Mhandisi Elias Mshana.
TRL Makao Makuu,
Dar es Salaam.
Machi 15, 2013

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...