Home
Unlabelled
BE THE FIRST TO KNOW...
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
Moja katika sera za serikali ya UK ni kuwa wauza chips wasikae karibu na shule. Sasa hapo wanafunzi wa Feza baada ya KFC kufunguliwa watanenepeana.
ReplyDeleteMDAU WA 12:31 UMENENA,TATIZO NYUMBANI HAWAANGALII HAYO MAMBO-INASIKITISHA SANA.
ReplyDeleteMDAU LONDON
Watanzania tunaenda wapi, tunakaribisha magonjwa ya nchi za dunia ya tatu, tutayaweza gharama zake? jamani ni gharama sana kutbia non-communicable diseases, sasa hayo ma KFC ya nini? Nchini Sweden hakuna KFC kabisa wanajali sana afya za watu wao. Jamani hizo kuku zimekaa mno na chips vyote vinawekewe preservatives, mdomoni vitamu ila madhara yake ni makubwa mnooooooooooo! Na ni ya maisha, embu tuendelee na vyakula vyetu wenyewe vya kujipikia majumbani. Hivi kwa nini wizara ya afya haishirikishwi kabla ya kuamua kuleta na kufungua biashara zitazoleta madhara kwenye miili ya watu? Hii ni biashara ila mwishio wa siku inaleta madhara sana. ma-Obesity ni mabaya sana kwa watoto, ona wamarekani wengi walivyo na Obesity na wanatembea na mavidonge meengi kushina kunywa madawa kila siku. Wizara ya Afya mko wapi? Bishara za vyakula ziangaliwe hasa zenye kulete madhara katika afya. Hivi sio vyakula ni magonjwa tupu. Wasioelewa hivyo watazidi kuugua, heri wanaofahamu madhara yake.
ReplyDeleteHIZO COMMENTS MBILI HAPO JUU USIZIBANIE NI KWA FAIDA YA WASIOJUA HIVYO. TAFADHALI SANA ZIWEKE.
ReplyDeleteMakubwa KFC ya nini bongo? Vyakula vyetu ni vizuri zaidi.
ReplyDeleteNyie wa hapo JUU mbona chips mavumbi zinauzwa mashuleni. na watumia mafuta kwa muda mrefu! Na mnao wasema wamerekani nina watoto wawili chochote wanachokula wanakuuliza kama ni cha AFYA. ukiwapa juice na maji watakunywa maji. Jee!! mtoto wa bongo atakimbilia nini kama sio juice , hawajawi kunywa soda!! or kula pipi walikuja bongo wakashangaa watoto wanakunywa soda. watoto wakimarekani wameelimika.
ReplyDeleteMdau wa kwanza unanena sawa kuhusu maobesity kwa mashule yetu hasa shule za watoto wa mafisadi. pia tatizo si obesity tu kuna watoto kuhadaiwa na mafisadi wenye uchu na watoto wa kike nafuu hizo chipsi zetu. KFC tamu ila ghali sana hapa watoto watahadaiwa mno mno.nadhani mnanipata.La pili mmmhh Mwai kibaki ndo barabara gani? kwa lipi? bado kuna postcode zinakuja utaona naming yetu inavyokuja.mi ningeomba serikali iwaaangalie watu wanaotoa mchango mkubwa kwa jamii yetu ila wasiwe na elements za ufisadi ndo tuwaweke kwenya kumbukumbu za mitaa na barabara zetu.asante hope michuzi hutaniweka kapuni.
ReplyDeleteninavyo fahamu KFC inategemea na wapi wanaweka branchi yao UK uarabuni KFC zote HALAL uk 10%HALAL TENA LONDON TU,jeee? bongo mnasemaje itakuwa HALALI AU ATALALA,NAJUWACHENI NA SWALI LANGU LKN KUKU WAKE WATAMUUUU mhhh
ReplyDeleteSASA JAMANI WABONGO, NAONA MMEANZA KUKOSOA! MBONA HAMPENDI MAENDELEO?KILA KITU KINACHOFANYIKA BONGO KIPYA NI KIBAYA ,SASA MNAONA ZILE CHIPS ZA AMERIKAN CHIPS KWA MANYANYA KINONDONI KWENYE UCHAFU LUKUKI, NZI ,VUMBI,MATOPE,MAVI MIKOJO, KUKU WALIOKWISHA OZA, WAPISHI WASIO KUWA NA AFYA, MAFUTA YA WIZI YA TRANSFORMER ZA UMEME NDIO WANAKANGIA MBONA HAMJASEMA? ...NA WEWE MDAU WA SWEDEN SIJUI NINI HUKO SWEDEN NDIO UMEONA NCHI PEKEE WEWE ULITOKEA WAPI KABLA HUJAENDA HUKO SWEDEN SIO TANZANIA AU HUKUWAHI KULA CHIPS KUKU AU CHIPS MAYAIM HUKU BONGO?
ReplyDeleteULAYA YOTE KUNA KFC, DENMARK IPO, GERMANY , FRANCE, UK, HOLLAND, JAPAN HATA CHINA WAKO WEWE UMEONA MFANO NI SWEDEN PEKE YAKE ? ACHA USHAMBA AU ULIJILIPUA HUKO 1 achane na nchi yetu iendelee mbona hamsemi kitu kuhusu STEERS.
ACHA TULE TUKIFA NI JUU YETU KWANI NINI CHA KUSHANGAZA KIFO KWA MUAFRIKA. WATU KAMA NYIE NDIO MAFALA MALIMBUKENI MKIFIKA HUKO MNAJIFANYA MMEISHAKUWA WAZUNGU KALABACHOLI, WALA HAMUWEZI KUFITI SOCIETY HIZO MNAJILAZIMISHA SHENZI TAIP.
BONGO OYEE, KAENI HUKO HUKO SWEDEN NA MSIRUDI HUKU
Walioandika hizi comments ni hakika wako nje ya nchi na wanaelewa vizuri matatizo yanayoletwa na hawa akina Kentuky na Mc D, lakini kumbukeni kuwa kuna nafasi kubwa katika huu ubia wa hii franchise wale wanaoitwa viongozi usishangae kukuta wanashare na ukisikia hao wanaojiita "Middle Class" watakwambia hayo ni maendeleo pamoja na "vikwangua anga" vinavyoporomoka na kuua watu yote ni maendeleo, tatizo kubwa la hapa nyumbani kwetu ni ubinafsi, hakuna uwajibikaji na viongozi wasio na upeo na wakifanya makosa hakuna wakuwauliza matokeo wanajiona miungu watu. HATUHITAJI KENTUKY DAR CHIPS ZA WAGOSI NA WALE JAMAA ZETUI WA KIHINDI PALE KISUTU ZINATOSHA Kamalizeni wamagharibi wenzenu.
ReplyDeleteJamaa wadau #1,2,3 mnaongea point sana.
ReplyDeleteLakini sie wabongo ubongo umeganda, wengi watakwambia nyie jamaa wa Ughabuni wacheni kujifanya mnajua-ndiyo majibu yao badala ya kupima mjadala. Ndiyo maana tunasema kwa Kiswahili chetu hicho,"tembea uone"
Nami Naungana na waliochangia kuwa haya ni maradhi. Kuna umuhimu wa kutoa tahadhari kama za sigara na pombe kwa hili pia. Athari nyingine ni zile za kampuni za simu za kutoa promosheni za ongea hadi asubuhi. Walengwa hapa si Watu wazima ila watoto wa shule na wale wa kipato cha chini. Basi utakuta usiku kucha wanaongea. Je hayo mafanikio ya masomo na tija ya kazi it's kuwepo kweli? Mara nyingi bure si bure kweli bali gharama tupu! Watanzania tujijali ! !
ReplyDeleteAma kweli! Ni ishara ya "maendeleo."
ReplyDeleteNiongezee: Kikwete na kabineti yako ikiwa ni pamoja na Tanzania Investment Centre, yYaani hatuwezi kufungua TFC yetu wenyewe tukitunia kuku wetu, kwa faida yetu?
Huo ni mrija mwingine wa kufyonza pesa zetu kuzihamishia bahari kubwa ya Amerika!
HE HE HE, JUZI HAPA TU MMAREKANI MMOJA ANA HAMBURGER YA MCDONALD ANAYO KWA MIAKA 14! HATA SISIMIZI, FUNGUS,KUNGURU WEUSI, ALKAIDA WAMEGOMA KULA HIYO BURGER, WAKE UP GUYS.
ReplyDeletekwa raha zenu wabongoo chips kuku za kfc ni tamujeee macdonald cha mtoto, yaani kfc chicken ni tamu balaa labda tuu wachakachue lakini kama watatengeneza kwa viwango vya huku majuu mtainjoy sana tuuu. na nyie hapo juu sio mjifanye mnajua saana mambo ya obesity watu wakinenepeana wataenda gym!
ReplyDeletemdau canada
Well well! Kwa ninavyofahamu au kiutmaduni unene au kuwa na mwili mkubwa ndio sifa ya Kiafrika au sijui niseme Kitanzania. Ukiwa na mtoto kibonge basi wewe unaonekana mambo safi! Kuwalisha watoto chipsi na mayai ni kuoyesha utajii bila kujua tuwawekea hazina ya maradhi ukubwani!
ReplyDeleteSisemi zaidi lakini "wajinga ndio waliwao"
Wajinga ndio waliwao haswa! Uamnuazi wa kununua na kula ni wa mtu binafsi, ila wenye eimu ya kutosha kuhusu hizo KFC hawatathibutu kununua! Wa marekani naomba ujaribu kusoma ni nchi gani duniani inaongoza kwa Obesity? Mie nafahamu ni Marekani, acha kubisha bila kufanya any research. Kwa sasa wameshtuka ila ndio hivyo too late na wanao-suffer obesity na magonjwa yake ni marekani ndio wanaongoza, watu wanene kama nyumba wanapatikana marekani. Usitetee kitu chochote hapo, wanao wamejua ubaya wa hivyo vyakula ila sio marekani inaongongoza kwa kula majunk food. Nenda uka google then uje uweke hapa ulichosoma. Watu wameathirika sana na sasa ndio wanashtuka though bado wanauza hivyo vyakula. Wacha tujilie zetu vyakula vyetu vya kitanzania kwani shida iko wapi? Wenye kuopt KFC kazi kwenu. Watanzania huwa hatuelimiki kirahisi ni wachache sana sana wanaelimika na kuelewa, majority ni fuata mkumbo. Jamani ndio mana mwisho wa siku tuna matatizo meeengi na ni ya kujitakia wenyewe.
ReplyDeleteKwa taarifa yako uliyeponda kuhusu Sweden, sasa ujue kuwa Sweden ni nchi ambayo inaongoza kwa watu wanaoishi miaka mingi duniani
ReplyDelete(Life expectancy yao iko juu sana) wanaishi miaka mingi. Kuna na Japan na ziko kama tatu tu zinazoongoza duniani.Fanya utafiti kabla ya kuandika vitu hapa. Wakati mwingine elimu inasaidia sana kuliko kutoa comments from the air!
Unene kwa watanzania ni sifa na kuonekana uko wealth, but its very unhealthy! Umbo la nje livutie watu wakati utakapoanza kusota na magonjwa unaanza kujutia huo unene! Unene kwa kifupi ni matatizo sana. Kama mnaweza ongeeni na Madaktari watawaambia mana hao wamesomea na wanaujua mwili wa binadamu vizuri. Nenda google angalia madhara ya kuwa mnene kila kitu kiko wazi. Ndio nasema watanzania hatuelimiki! ni wachache sana wanaelewa na kuelimika kukubali kubadilika.
ReplyDelete