Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad amesema Mhe. Fatma Ferej hakupendelewa kupewa tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania kwa mwaka 2013 bali amestahiki kutokana na utendaji wake.
Akizungumza katika hafla maalum ya kumpongeza Mhe. Fatma Fereji kutokana na kupewa tunzo hiyo na ubalozi wa Marekani nchini Tanzania tarehe 4/3/2013, Maalim Seif amesema Fatma Ferej ni mchapa kazi wa kweli na jasiri katika kutekeleza majukumu yake.
Amesema akiwa msaidizi wake katika Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais , Fatma Ferej amekuwa akimsaidia kwa karibu hasa katika kufuatilia masuala ya dawa za kulevya, mazingira na maendeleo ya watu wenye ulemavu.
Pia alimsifu kutokana na busara na mashirikiano yake na watendaji wengine wa Ofisi hiyo. “Sijawahi kupokea malalamiko kuwa Mhe. Fatma anawanyanyasa wafanyakazi wake, bali siku zote namuona ni kiongozi mwenye busara na mashirikiano makubwa”, alifahamisha Maalim Seif.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CUF Taifa Prof. Ibrahim Lipumba ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo alisema Tunzo aliyoipata Fatma Ferej imekijengea sifa kubwa chama chake cha CUF.
Prof. Lipumba alitumia fursa hiyo kuwaasa wazazi na walezi kutowabagua watoto wao na kuwapa fursa sawa za kielimu ili waweze kujiandaa vyema kukabiliana na maisha, sambamba na kuwapa fursa wanawake waweze kushiriki shughuli za kijamii.
Nae Mhe. Fatma Ferej amesema anaichukulia tunzo hiyo kama ni changamoto ya kuzidi ari ya kiutendaji, na kuwataka wanawake wajiamini wanapotekeleza majukumu yao.
Amefahamisha kuwa wakati umefika kwa wanawake kuuthibitishia ulimwengu kuwa wanaweza, na kuondokana na mtazamo finyu kuwa kazi za wanawake ni kukaa jikoni pekee.
Hafla hiyo ya pongezi maalum iliyofanyika hoteli ya Bwawani, iliandaliwa na Jumuiya ya wanawake wa CUF.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Mhe. Fatma Ferej kwa kupewa tunzo ya mwanamke jasiri, 2013.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba akimpongeza Fatma Ferej kwa kupewa Tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania kwa mwaka 2013.
Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar Maalim Seif Sharif Hamad, akizungumza katika hafla ya kumpongeza Mhe. Fatma Ferej kwa kupewa tunzo ya mwanamke jasiri, 2013.
Mwenyekiti wa CUF Prof. Ibrahim Lipumba akimpongeza Fatma Ferej kwa kupewa Tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania kwa mwaka 2013.
Viongozi wanawake wa CUF wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fatma Ferej (wa nne kulia) katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika hoteli ya Bwawani.
Viongozi wa CUF wakiwa katika picha ya pamoja na Mhe. Fatma Ferej (wa nne kulia) katika hafla ya kumpongeza iliyofanyika hoteli ya Bwawani.
Mke wa Makamu wa Kwanza wa Rais Mama Awena Sinani, akiangalia kazi za wajasiriamali wa CUF, akiongozana na Mhe. Fatma Ferej, katika hafla ya kumpongeza kutoana na kupewa tunzo ya mwanamke jasiri Tanzania 2013.
Wasanii wa ngoma ya Kingazija wakisubiri kutoa burudani katika hafla ya kumpongeza Fatma Ferej, hoteli ya Bwawani.
Chapeni kazi tutafika kwa uwezo wa Muumba. Cha msingi mujali uadilifu
ReplyDeleteHongera sana Fatuma, Hongereni pia viongozi wa CUF kwa kulitambua hilo.
ReplyDeleteMungu awaongoze vyema na awaongezee elimu nzuri na muendelee kuwa viongozi wanaojali haki daima.
Ankal heshima yako.Kwenye Ngoma uzipendazo ngoma za Kingazija hazimo?Ningependa kuiona inavyochezwa.Kama una clip yake.......Tafadhali Ankal
ReplyDeleteDavid V
Kwahio Ubalozi wa Marekani umempa huyu ndugu yetu tuzo na Chama chake imeona hicho ni kitu cha kutumia fedha na kufanyia sherehe kabisa?? Huku kutawaliwa kwa fikra kubaya sana!!
ReplyDelete