Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia wadudu wa ugonjwa wa Maralia kwa kwa kutumia Mashine ya Hadubini, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho wakati wa ufunguzi wa Mkutano wa pamoja wa Kimataifa wa Watafiti wanasayansi wa Afrika, alioufungua jana jijini Arusha. Picha Zote na OMR
Makamu wa Rais Dkt. Bilal,akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkuuwa Mawasiliano wa Kampuni ya Utafiti, Mafunzo na Huduma ya Ifakara Health Institute, David Mbulumi, wakati alipokuwa akitembelea Mabanda ya maonyesho katika mkutano huo jana.
Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akisikiliza maelezo wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika Mkutano huo, jana.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilali, akifungua rasmi Mkutano wa Pamoja wa Kimataifa wa Watafiti Wanasayasi Afrika ulioandaliwa na Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kwa kushirikiana na Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS) ya Afrika Kusini. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela. Mkutano huo wa siku nne unafanyika Jijini Arusha.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na  Dkt Martha Lemnge, baada ya kuwakabidhi tuzo zao hizo jana.
Makamu wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Bilal akiwa katika picha ya Pamoja na Washindi wa Tuzo za mwaka 2012 za Masuala ya Afya, Prof. Ester Mwaikambo (kushoto) na  Dkt Martha Lemnge, baada ya kuwakabidhi tuzo zao jana. Kulia ni Mkurugenzi wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela.
 Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu Tanzania (NIMR), Dkt. Mwele Malecela akisoma hotuba yake.
Sehemu ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali.
 Badhi ya Watafiti Wanasayansi kutoka Taasisi zaidi ya 35 barani Afrika wakimsikiliza kwa makini Mkurugenzi Mkuu wa NIMR wakati wa hotuba yake ya ukaribisho.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS), Mark Rweyemamu akisoma risala yake wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo Jijini Arusha.
Viongozi wa NIMR na Watafiti mbalimbali wakimsikiliza Mtendaji Mkuu wa SACIDS.
 Mkurugenzi wa OHCEA, Japhet Kilewo akitoa hotuba yake.
 Meza kuu ikifuatilia kwa ukaribu Hotuba ya Mkurugenzi wa OHCEA.
 Mwakilishi kutoka Umoja wa Afrika (AU)Dk. Ahmed Hamdy akizungumza na Wanasayansi watafiti.
  Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid nae alisoma Hotuba ya Wizara na kumkaribisha Mgeni Rasmi kufungua mkutano huo.
 Wakuu wa Taasisi za kitaifa na Kimataifa pamoja na wanasayansi watafiti wakifuatilia hotuba ya Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii.
 Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, pamoja na Mkurugenzi wa NIMR, Dkt. Mwele Malecela wakizindua rasmi awamu ya nne ya Vipaumbele vya Tafiti za Afya kwa mwaka 2013-2018.
 Pia Makamu wa Rais alipata fursa ya kuzindua Mpango wa Afya Moja nchini Tanzania.
Aidha Makamu wa Rais Dkt Mohammed Gharib Bilal, pia alizindua Mpango wa Uchunguzi wa Magonjwa ya Kuambukiza Kusini mwa Afrika (SACIDS).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Hongera sana mama Esther na mama mwingine....Naomba niulize: Hivi hivyo vidude ( nishani) vina gharama gani?

    Mini huwa nashindwa kuelewa...sisemei kwa hawa wamama...Utakuta mtu mwingine anapewa hicho kidude lakini ana shida kibao za pesa.Si bora wangekuwa wanawapa pesa pamoja na cheti cha sh 5000/=?

    Hii niliiona wakati wa maadhimisho ya miaka kadhaa kAIRUKI HOSPITAL.
    Kweli wengi waliopewa hicho kidude walikuwa na shida ya hela si vinginevyo. Mie niliweza kuwahoji baadhi ili nipate maoni yao . Wote walipendelea kupewa pesa badala ya hivyo vidude

    ReplyDelete
  2. Very nice to see Prof Japhet Killewo on board. You have always inspired me in the field of public health and epidemiology

    ReplyDelete
  3. Safi sana Prof. Rweyemamu! Ulitakiwa kuwa waziri wetu wa kilimo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...