Kutokana na maombi ya wengi, Globu ya Jamii inatii amri ya wadau ya kuanzisha makala ya KUTOKA MAKTABA itayoenda sambamba na Ngoma Azipendazo Ankal kila siku. Kwa kuanzia hapa ni Mnazi Mmoja jijini Dar es salaam mwaka 1990 wakati wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Jangwani walipojiunga na maelfu ya wananchi kumpokea Nelson Mandela alipotembelea Tanzania mara tu baada ya kuachiwa huru.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Ahsante mkuu kwa kutuwekea uhondo huu wa picha hasa ukizingatia nyingi umepiga ww so utazitolea maelezo ya kina.

    kwa picha hii ya kwanza ya ujio wa Nelson Mandela inanikumbusha nikiwa darasa la pili pale Arusha School, nje ya New Arusha Hotel tulijipanga kando ya barabara na bendera za SA & TZ. Ulikua ujio wa kishujaa hasa ikizingatiwa ni baada ya kutoka gerezani

    ReplyDelete
  2. Aise namuona FAtma Fereji kwa Mbele

    ReplyDelete
  3. kwa kweli tushazeeka uncle, mwaka tisini wengine ndo wako la pili.

    ReplyDelete
  4. nilikuwepo siku hiyo na nilibahatika kumuona mzee madiba

    ReplyDelete
  5. safi sana,kuna picha ankal ulipiga ikulu koffi Annan alipokuja TZ mwaka 98.katika wale jamaa wakitoa huduma na vikoti vyekundu nilikuwemo kaka siku moja nadhani ntaziona hizo hapa.

    ReplyDelete
  6. Sasa huyo mwenye Baisikeli na msuli kiunoni ndio nani?

    Ama ni Mwalimu wa Sekondari JANGWANI?

    ReplyDelete
  7. Picha za namna hii zinaliza wengi, hiyo tokea mwaka 1990.

    Wanao fahamiana hapo watajua miongoni mwao ni kuwa:

    1.Wapo walio tangulia kwa Mwenyezi kitambo tu.

    2.Maisha ni tambara bovu hapo wapo ambao maisha yao hali zao ni Mwenyezi anajua, huku wakiiona picha hio watalia wakikumbuka enzi hizo.

    3.Wapo ambao mambo yao ni Neema kwa neema.

    Siri ya maisha aijuaye ni Mwenyezi pekee.

    Kweli maisha kitendawili!

    ReplyDelete
  8. kweli inakumbusha mbali huo ni miongoni mwa mikusanyiko mikubwa iliyowahi kutokea dar es salaam.ujio wa mandela na ulinganisha na mapokezi ya simba baada ya kutwaa kombe la challenge zanzibar.siku hizi mbili zilifanya en la posta liwe halipitiki kabisa.hata pakukanyaga ilikuwa shida.haya ni miogoni mwa matukio mawili yaliokuwa na umati mkubwa sijapata kuuona labda yalizidiwa na umati wa msiba wa baba wa taifa.

    ReplyDelete
  9. Kwakweli siku hiyo uvumilivu ulinishinda, mvua ilinyesha sana, nakumbuka nilikuwepo hapo nikiwa kidato cha kwanza Jangwani.Huyo mwenye baiskerli si mwalimu wa Jangwani. Jangwani oyeeeeeeeeeeeeee!!!!!!!!
    Jangwani shule yetu,
    Jangwani twaipenda,
    Jangwani yasifikia popote Tanzania,
    JENGA, JIHESHIMU, JITEGEMEE NI MOTO WA SHULE YETU. Wimbo wetu wa shule ukiongozwa na Mwalimu Mkichwe enzi hizo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...