Jengo la ghorofa nane lililokuwa na viwanda vya nguo na maduka limeporomoka leo mchana nje ya jiji la Dhaka, Bangladesh, na kuua watu takriban 100 na kujeruhi wengine zaidi ya 1000, maafisa wamesema.
Vikosi vya zimamoto na askari jeshi wanaendelea kufukua vifusi vya jengo hilo lililo maeneo ya Savar, ya jiji la Dhaka. TV zimeonesha wafanyakazi wanawake wakiokolewa wengi wakiwa wamepoteza fahamu. Askari wa zimamoto mmoja amenukuliwa akisema takriban watu 2000 walikuwamo mjengoni wakati linaporomoka
Biashara ya nguo ya Bangladesh imekumbwa na majanga ya moto na ajali zingine kwa miaka kadhaa, licha ya juhudi za kuboresha usalama pahala pa kazi. Mwezi Novemba mwaka jana wafanyakazi 112 walikufa katika mlipuko katika kiwanda cha nguo na kuzua mkanganyiko kwa wafanyabaishara wa kimataifa wa nguo wanaopata bidhaa hiyo Bangladesh.
Afisa mmoja katika chumba cha mikakati ya uokoaji kilichowekwa ili kutoa taarifa kwa watu, alisema watu 96 walikuwa wamethibitishwa kufa na zaidi ya 1000 kujeruhiwa. Madaktari katika hospitali za jirani wamekiri kuzidiwa na majeruhi walioletwa kwao.
Mkuu wa polisi wa eneo hilo, Mohammad Asaduzzaman, alisema wamiliki wa viwanda hivyo vya nguo mjengoni humo walidharau onyo la kutoruhusu wafanyakazi mjengoni baada ya nyufa kuonekana katika baadhi ya kuta jana. Katika jengo hilo mlikuwa na viwanda vitano vilivyoajiri zaidi kinamama.
TBS kueni macho na nondo za vyuma chakavu, la sivyo majanga haya hayatakoma.
ReplyDeleteRushwa na Mipango ni Dunia nzima.
ReplyDeleteHivi na hapo ni Dar Es Salaam?
Lilipoanguka ghorofa lawama zilikuwa kwa Kiwete, Chama na Serikali!
Sasa je na hapo ni Tanzania?
Rushwa na Ufisadi ni tatizo la dunia nzima, angalieni mifano hii ktk nchi kama hizi:
1.Italia aliyekuwa Waziri Mkuu Bilionea Silvio Berlusconi anatumikia Kifungo cha miaka 4 Jela kwa Rushwa na Ufisadi.
2.Kansela Angel Markel wa Ujerumani amemlaumu Raisi wa Klabu kubwa ya Mpira nchini humo kwa kukwepa Kodi.
Je na hapo No.1 na No.2 jamaa wapo Tanzania na Raisi wa nchi zao ni Kikwete?
Ehhh TBS tena hapo!
ReplyDeleteWewe Mdau wa kwanza hapo sio Dar Es Salaam na wala sio Tanzania!
Suala liko pale pale. Kiongozi ndiye muwajibikaji. Penye Ufisadi, Rushwa, Miundo mbinu mibovu, nk. Kiongozi ndiye msababishaji kuendana na aina na namna ya uongozi wake!
ReplyDeleteNa hapo ni Bangladesh ghorofa limeporomoka analaumiwa tena Kikwete wa Tanzania, Chama na Serikali???
ReplyDeleteMdau wa nne juu anony Thu Apr 25, 03:59:00 pm 2013
Sasa Kiongozi atasababisha vipi kwani yeye ndie Fundi?