Spika wa Bunge Anne Makinda awaasa Wabunge kutumia Lugha ya Staha ambayo ni ya Kibunge wakati wa kuchangia mijadala Bungeni. Mhe. Makinda amesema, kuendelea kutumia lugha ya matusi, kejeli na maudhi kwa baadhi ya Waheshimiwa Wabunge ni kuendelea kuliondolea hadhi Bunge. 

Pamoja na hilo, wabunge wanatakiwa kujikita katika kuchangia hoja zenye kutataua matatizo ya wananchi ili kutimiza wajibu wa kila mbunge wa kuwa wakilisha wananchi. Mhe. Makinda , amesema, fursa ya kila Mbunge kuchangia lazima ilenge kutatua matatizo ya wananchi na sio kutukanana na kusahahu jukumu lilomblele ya kila Mbunge. 

Katika Picha ni baadhi ya waheshimiwa Wabunge waliochangia mjadala wa kupitisha Makadirio na Matumizi ya Ofisi ya Waziri Mkuu na Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2013/14 Bungeni Mjini Dodoma leo. Picha zote na Owend David wa Bunge
Spika wa Bunge Mhe. Anne Makinda akiwaasa Waheshimiwa Wabunge kutumia Lugha ya Kistaarabu kuchangia mijadala Bungeni.
Mbunge wa Mwibara Mhe. Kangi Lugola, akiomba Mwongozo kwa Spika Bungeni
Mhe. Catherine Magige, Mbunge wa Viti Maalum (CCM) akichangia Mjadala leo
Mbunge wa Temeke Mhe. Abbas Mtembu akichangia Mjadala
Mbunge wa Ukerewe Mhe. Salvatory Machemli akichangia Mjadala Bungeni leo
 Mbunge wa Viti Maalum (CUF) Mhe. Kuruthum Mchuchuli akichangia  kwa hisia mjadala leo Bungeni.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na teknolojia Mhe. January Makamba akijibu baadhi ya hoja zilizochangiwa Bungeni leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. NAOMBA KUELIMISHWA KUHUSU VILE VIPAZA SAUTI KULE BUNGENI, BILA KUVIINAMIA HUSIKIKI? KAMA JIBU NI NDIO KWA NINI VIKAWEKWA VIFUPI? NA KAMA JIBU NI HAPANA KWA NINI WABUNGE HAWAFUNDISHWI WANAPOINGIA BUNGENI KWA MARA YA KWANZA KUHUSU MATUMIZI YAKE PAMOJA NA VIFAA VINGINE? MPAKA WAMALIZE VIPINDI VYAO MIGONGO ITAWAPINDA.

    ReplyDelete
  2. Can someone educate me please. Why these law makers have to flex their upper body muscles and spend so much energy while speaking? Why can't they just relax and speak in a calm way? Are the microphones not powerful enough to amplify their voices? Thanks

    ReplyDelete
  3. New technology to backward MPs.

    ReplyDelete
  4. hahahah...pinda mugongo hadi bungeni!

    ReplyDelete
  5. tatizo sio technology ila umeme ulikuwa wa mgao, hivyo ikabidi wajipinde tu ili wasikike ahahahah

    ReplyDelete
  6. Wanafunzi na wataalamu wa media ecology, mtakumbuka ya Marshall McLuhan kuhusu hot and cool media:

    Paraphrased: His famous distinction between "hot" and "cool" media referred to the different sensory effects associated with media of higher or lower definition. High-definition ("hot") media, such as print or radio, are full of information and allow for less sensory completion or involvement on the part of the reader or listener than low-definition ("cool") media, such as telephone or television, which are relatively lacking in information and require a higher sensory involvement of the user. The form of each medium is associated with a different arrangement, or ratio, in the order among the senses and thus creates new forms of awareness. These transformations of perceptions are the bases of the meaning of the message. In this sense, "the medium is the message."

    Ukiwasikiliza kupitia radio au mkutano wa hadhhara, wanaonekana wakiunguruma sana. Lakini kupitia luninga, wanatisha!

    Anyway, both a radio and mkutano wa hadhara are hot media; environment. Na ya bungeni kwa kuzungumzza kupitia vipaza sauti au kuwaona kwenye luninga wanajikita katika environmment za cool media.
    Hawana haja ya kufunzwa hayo matumizi tofauti.

    Wataalamu wa media ecology (studies in media) wanaamini kuwa Hitler alifaa sana kwa radio; luninga ingemwangusha vibaya kwani angeeonekana anatisha!

    ReplyDelete
  7. eeeeeehhh kiti maaalumu mh catherine! nyumbani kuzuri bwana ankali em fanya fanya basi utubandikie ya mheshimiwa vicky kamata

    ReplyDelete
  8. waache ujinga wafanye kazi alaaah.
    hawakumbuki muda na nguvu zetu tulizotumia kuwapigia kura.
    wamejisahau kuwa hapo wapo kwaajili ya watanzania wote na wakumbuke tumewatuma ni kazi na si mzaha kama wanavofikiria

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...