Habari Ankal,
Leo katika pita pita zangu za kila siku,nilibahatika kupita barabara ya Msasani ambapo ni karibu kabisa na kituo cha Daladala cha Tido na kukutana na kitu ambacho sikuweza kuamini baada ya kuona kwa macho yangu ya kawaida,kwani niliona lori (semtrela) likipiga utani moja matata na kupelekea sisi wengine wenye mikoko ya mikopo,kusimama ili kusubiria mtaalam huyo apige hiyo yutani yake.hapa ndipo nilipoanza kujiuliza lile swali la kuwa,magari makubwa ya namna hii kwanini yanaruhusiwa kuingia maeneo ya katikati ya mji nyakati za mchana??Wadau namba mnisaidie katika hil.
Mdau wa Ukweli wa Globu ya Jamii
Tumeshachoka na matatizo yenu huko Bongo, kila siku hili mara lile watu kama sio binadamu bwana wanashindwa kufikiri vitu vidogo tu. Ma uchafu kila kona, watu wanajijengea tu ovyovyo hakuna mipangilio ya maisha.Hata wanyama wana afadhali. shida mpka kwenye nyuso, rushwa, ufisadi, watawala jeuri!! Tunawaombea kwa Mungu na nchi yenu hiyo !!
ReplyDeleteMdau kituo cha daladala kinafahamika kwa jina la TIRDO na sio TIDO.
ReplyDelete