![]() |
| Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas |
Na Veronica Kazimoto – MAELEZO
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limekanusha taarifa ya kuachiwa huru kwa mtuhumiwa wa ujangili Bw. Frank William Silangei maarufu kwa jina la “Ojung’s Mwarusha” mkazi wa Ngaramtoni Kibaoni iliyotolewa na gazeti moja la kila wiki.
Akizungumza katika mahojiano kwa njia ya simu na Idara ya habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, Kamanda wa polisi mkoa wa Arusha Liberatus Sabas amesema kuwa mtuhumiwa huyo mwenye umri wa miaka 32 hivi sasa yuko mahabusu na taratibu za kumfikisha mahakamani zinaendelea kufanyika.
Kamanda Sabas ameeleza kuwa mtuhumiwa Silangei hajaachiwa huru kama ilivyoripotiwa na gazeti hilo linalotoka kila Alhamis katika ukurasa wake wa kwanza na wa pili na kuongeza kuwa Jeshi la Polisi mkoani humo liko makini katika kutekeleza majukumu yake.
“Si kweli hajaachiwa, natamani ungekuwa hapa Arusha nikakupeleka mahabusu ukamuona mtuhumiwa kwa macho yako”, amesema Kamanda Sabas.
Kamanda Liberatus Sabas amesema Serikali kupitia Jeshi la Polisi itaendelea na jitihada zake za kuhakikisha kuwa vitendo vyote vya ujangili vinatokomezwa na yeyote atakayehusika na vitendo hivyo atachukuliwa hatua za kisheria.



Mie nasema hivi, tunataka kuona amani na utulivu Arusha inasisitizwa na wahalifu woote wanao vuruga Arusha ambayo hapo awali ilikuwa tulivu sana, watu tukienda teka maji saa mbili usiku bila woga ila sasa ikipita saa kumi na mbili unaogopa kuvamiwa au kulipuliwa risasi na majangili!!! kwakweli jeshi la police mkoani Arusha tunawaomba muendelee kuwa bana wahalifu mpaka wakome kabisa. Fagia woote kabisa watuachie Arusha yeetu. Mungu awabariki sana Jeshi la Police, mkuu wa mkoa na wananchi woote kwa ujumla.
ReplyDeleteNaomba Kamanda wa jeshi, mkuu wa mkoa wa Arusha na wana nchi woote tushirikiane kwa nguvu zoote ili kuwaondoa majambazi woote wanachafua jiji la Arusha!! kwakweli Arusha hii ya sasa hivi haifurahishi kabisa, matendo ya kijambazi na wezi wametanda kila kona mjini Arusha!! Police wachapeni woote wanao vuruga amani na mkuu wa mkoa simama Imara kabisa usikubali kuyumbishwa na wana nchi watajeni woote wanao leta tabia za uhalifu jijini humu. Msiwafiche.
ReplyDeleteNa polisi wenyewe watambuane ni wepi waharifu na wepi waadilifu. Maana tunaweza kujidanganya kuwa jeshi la polisi linajitahidi kudhibiti lakni linashindwa labda kutokana na wahalifu kuwa ndani ya jeshi hilo kama tunavyosikia.
ReplyDelete