SHIRIKA la Kijerumani la Friedrich Ebert Stiftung (FES), limekipongeza na kukisifu Chama Cha Mapinduzi (CCM), kwa kuendelea kujenga utawala bora na kujenga amani ya nchi.

Akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM, Bara, Philip Mangula,Mkurugenzi Mkazi wa FES nchini, Rolf Paasch, alisema shirika lake linatambua juhudi na kazi inayofanywa na CCM katika ujenzi wa demokrasia na amni ya Tanzania.

Paasch alisema Tanzania ni nchi muhimu katika historia ya bara la Afrika hususan mchango wake katika ukombozi wa nchi zilizo kusini mwa Afrika, hivyo inapaswa kuwa mfano na kuhifadhi kumbukumbu muhimu za kihistoria kuhusu ukombozi.

"Ni mara yangu ya kwanza kuja Tanzania na nafurahi leo kukutana nawe kiongozi wa juu wa CCM, kwa niaba ya FES naahidi kuimarisha na kuedndeleza ushirikiano uliopo baina yetu na CCM na Tanzania kwa jumla," alisema.

Kwa Upande wake Mangula, alisema katika kuhakikisha Tanzania inatunza kumbukumbu muhimu za kihistoria za bara la Afrika, kwa makubaliano na nchi zingine za bara hilo zimeamua kutenga eneo maalumu wilayani Bagamoyo kwa ajili ya ujenzi wa kijiji cha kumbukumbu hiyo.

Mangula alimwambia mkurungenzi mkazi huyo kuwa tayari eneo hilo limeshapatikana na kwamba mchakato wa hatua zaidi katika kuelekea ujenzi wake kwa kushirikiana na nchi nyingine, unaendelea

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...