WIZARA yua ujenzi imetoa mafunzo kwa wanawake wakandarasi kuhusu njia ambayo inaweza kuwasaidia kushiriki kikamilifu katika kazi za ujenzi za Barabara ambapo imebainika kwamba wanawake wengi wakandarasi hukumbana na changamoto nyingi katika kazi za ujenzi kutokana na uwepo wa ushindani mkubwa kwa sasa.

Hayo yamebainishwa leo katika semina ya mafunzo ya IZARA ya Ujenzi, Barabara na Nyumba na kutoa uwezo kwa wahandisi wanawake kushiriki kikamilifu katika kazi za barabarani yaliyofanyika katika ukumbi wa Kilimanjaro Cranes na kushirikisha washiriki zaidi ya 30 kutoka katika mikoa zaidi kumi.
Meneja wa TANROAD mkoa wa Kilimanjaro, Marwa Rubirya akizungumza na Washiriki katika ufunguzi wa Semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa Kiliamnajro Cranes kutoa mafunzo ya ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za Barabara nchini.
Kaimu katibu Tawala wa Mkoa wa Kilimanjaro, Martha Ufunguo, akizindua semina ya mafunzo ya siku kumi kwa Washiriki zaidi ya 30 yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi kutoa mafunzo ya ushirikishwaji wa wanawake katika kazi barabara, yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Kilimanjaro Cranes, mkoani Kilimanjaro.
Katika picha ya pamoja ni washiriki wa semina ya siku ya mafunzo ya ushirikishwaji wa wakandarasi wanawake katika kazi za barabrani, kutoka katika mikoa ya Kilimanjaro, Tanga, Geita, Manyara, Arusha, Singida, Da es salaam, Katavi na Pemba, yaliyoandaliwa na Wizara ya Ujenzi, katikia ukumbi wa Kilimanjaro Cranes, Mkoani Kilimanjaro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...