Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akipokea fimbo ya Kitemi kutoka kwa  Antonia Mipamo maarufu kwa jina la Tonisiza ambaye pia ni Mtemi Chigoku Masa wa Simiu baada ya  kutawazwa muwa Mtemi wa Wasukuma wakati alipozindua sherehe za Utamaduni wa Wasukuma katika uwanja wa Bujora, Kisese jijini Mwanza Juni 2, 2013.
 Baadhi ya watemi wa Kisukuma wakiingia kwenye Kituo cha Utamaduni wa kabila la Wasukuma cha Bujora kilichopo Kisesa Mwanza ambako sherehe za  Utamaduni  wa wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo zilifanyika Juni 2, 2013.
  Baadhi ya washiriki wa sherehe za  umtamaduni wa Wasukuma maarufu kwa jina la Bulabo wakimsikiliza Waziri Mkuu, Mizengo Pinda wakati alipohutubia alipozindua sherehe hizo kwene uwanja wa Bujora Kisesa jijini , Mwanza  juni 2, 2013.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. AnonymousJune 03, 2013

    Ni vizuri sana kuwa na sherehe kama hizo kila mwaka baada ya mavuno.Mimi nilizaliwa na kuishi miaka 35 iliyopita.Je nitaweza kupata wapi hotuba za Kisukuma au ngoma za utamaduni wa kabila hilo. Hivi PM aliongea kwa lugha gani ktk sherehe hizo?

    ReplyDelete
  2. AnonymousJune 03, 2013

    Duhhh Mila zenye faida tamu sana!

    Tutafurahi kuwaona vijana wa kisasa na visu vya viunoni huku wakiwa na Migolole badala ya kuvaa suruali za Modo.

    Hubu ngalieni Waheshimiwa walivyopedneza na Majoho ya Kiasilia, kwa nini Mabrazameni na Masharo baro wetu vijana wasichukue mwenendo huo na badala yake kukurupukia Mambo ya Utamaduni na mila za nje?

    ReplyDelete
  3. AnonymousJune 03, 2013

    Utaratibu huu wa Mila na Utamaduni ungefaa sana kuwepo ktk Mashindano ya Urembo ya Miss Tanzania.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...