WIZARA ya Maliasili na Utalii inawashukuru watu wote waliotembelea Banda la Maliasili na Utalii katika Viwanja vya Sabasaba jijini Dar es Salam na kutuwezesha kuibuka mshindi wa Kwanza wa Banda Bora katika kundi la Taasisi za Serikali zilizoshiriki katika maonyesho ya Kimataifa ya 37 ya Saba Saba 2013. 
Ushindi huu unaama kubwa sana kwetu kwani haikuwa rahisi kuhakikisha wananchi waliokuwa wakiingia kwa wengi bandani kwetu wanapata elimu yakutosha kutoka kwa wataalamu na wadau mbalimbali wa sekta ya utalii, wanyamapori na mambo ya kale waliokuwa wakitoa elimu mbalimbali zikiwemo za uhifadhi endelevu wa wanyamapori, ufugaji nyuki na utalii. 
Aidha wale ambao hawakujaaliwa kwa sababu moja ama nyingine kufika kwenye banda letu wasiwe na wasiwasi wanaweza kuungana nasi kwenye Maonyesho ya Nanenane Dodoma ambapo tutahakikisha tunafanya vema zaidi. 
 Sambamba na hilo Wizara inachukua fursa hii kuomba radhi kwa wale wote wailiokwazika kwa namna yoyote ile katika kipindi chote cha Maonyesho ya Kimataifa ya Biashara 37 kwani tunatambua wananchi wengi mlikuwa na kiu ya kutembelea banda la wanyama hai hata muda ambao tulilazimika kulifunga (saa kumi na mbili jioni) kutoa fursa kwa wanyama kupumzika na kupata mlo wao wa usiku. Mwisho kabisa Wizara inawatakia Ramadhani Kareeem wale wote waliofunga na Mwenyezi Mungu awajaalie kila la heri katika mwezi huu mtukufu Amin.
 BAADHI YA WATENDAJI WAKUU NA MAAFISA WAANDAMIZI WA WIZARA YA MALIASILI NA UTALII WAKIWASHUKURU WANANCHI MBALIMBALI WALIOKUWA WANAPITA NJE YA BANDA LA MALIASILI NA UTALII KWENYE MAONYESHO YA 37 YA KIMATAIFA YA BIASHARA MWAKA HUU KWA KUWAPUNGIA MIKONO NA KUWAONYESHA MOJA KATI YA TUNZO WALIZOZIPATA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 11, 2013

    Hongereni.Mwaka kesho jitahidini kumleta mzee wa mbio-DUMA(Cheetah)....

    Watanzania:Tujitahidi kutembelea mbuga "ORIJINO' kuliko kusubiri/kubanana/kupigana vikumbo kwenye hizi artificial parks za maonyesho ya Saba saba.

    David V

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...