
Miss
Tanzania 2012, Brigitte Alfred (kulia)
akipokea hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 4.1 kutoka kwa Mkuu wa
Kitengo
cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC),
Susan
Omari jijini Dar es Salaam jana. Fedha hizo ni kwaajili ya ujenzi wa
Bweni la
wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi (Albino) linalojengwa katika shule ya
Msingi
Buhangija mkoani Shinyanga. Fedha hizo ni maalum kwaajili ya kununulia
mabati ya kuezekea bweni hilo. Kwa mujibu wa Brigitte zaidi ya Shilingi
milioni 60 zinahitajika kukamilisha ujenzi huo.
Unless I am missing something,there should never be separate dormitories for such children! Could someone please explain this seemingly "positive discrimination" to me?
ReplyDeleteNakuunga mkono Brigitte kwa uamuzi mzuri wa kuwajali watoto hawa wa Buhangija Albino's Centre. Natoa wito kwa watanzania wenzangu mlioko ndani na nje ya nchi kuchangia jitihata za binti huyu mwenye moyo wa pekee.
ReplyDeleteHaya shime wana Buhangija, Shinyanga na watanzania wote kwa ujumla. Msaada wetu unahitajika sana ktk kuendeleza kituo hiki muhimu kwa watoto wetu wenye mahitaji haya.
Mkereketwa wa Buhangija Albino's Centre.