Rais Barack Obama wa Marekani ameondoka nchini mchana huu kurudi nchini Marekani,baada ya kumaliza ziara yake ya siku mbili hapa nchini iliyoanza jana.Rais Obama na mwenyezi wake Rais Jakaya Kikwete, leo walifanya ziara ya kutembelea mitambo ya kuzalisha umeme ya Symbion iliopo Ubungo jijini Dar es Salaam ambako Rais Obama alizindua rasmi mpango wa nchi yake kusaidia upatikanaji wa umeme wa uhakika kwa nchi saba za Afrika, ikiwemo Tanzania.

PICHA ZA MATUKIO MBALI MBALI ZITAWAJIA BAADAE KIDOGO 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. AnonymousJuly 02, 2013

    Asante Ankal mana wadau Diaspora tunazisubiri picha na video clips kwa hamu.
    MAM

    ReplyDelete
  2. AnonymousJuly 02, 2013

    TUWEKEE SASA

    MDAU -CM

    ReplyDelete
  3. AnonymousJuly 02, 2013

    Michuzi nadhani muda umefika inabidi uwafukuze kazi baadhi ya wafanyakazi wako kwa matumizi mabaya ya lugha. Utasemaje Rais obama wa marekani? kwani kuna Rais obama wa nchi nyengine duniani? Kiswahilisanifu ni ama rais obama au rais wa marekani full stop.

    ReplyDelete
  4. AnonymousJuly 02, 2013

    Anasahihisha kiswahili, huku anaandika "nchi nyengine".

    Kazi ipo.

    ReplyDelete
  5. AnonymousJuly 02, 2013

    Ziara imeenda vizuri ila mbona hizo barabara zetu zina mchanga mwingi, mameya hamuwezi kuweka usafi na kuondoa huo mchanga? JK amejitahidi sana ila mji bado mchafu. Jitahidini wahusika kurekebisha mji wetu.

    ReplyDelete
  6. AnonymousJuly 02, 2013

    Ziara ya siku mbili au masaa?siku ni masaa 24,huyu bwana hakutimiza

    ReplyDelete
  7. AnonymousJuly 04, 2013

    ni sawa ni 48, jumlisha na yale kwenye ndege kuingia na kutoka nchini

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...