Rais Barrack Obama wa Marekani na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakizungumza na watendaji wa kuu wa sekta ya umeme nchini.Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini Mr.Maswi,mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam Sadik Meck Sadik na watatu kushoto ni Waziri wa Nishati na Madini Profesa Sospeter Muhongo wakati kiongozi huyo wa Marekani alipotembelea mradi wa kuzalisha umeme unaofanywa na kampuni ya Symbion power ya Marekani huko Ubungo jijini Dar es Salaam leo.

Rais Barack Obama wa Marekani akizungumza jambo na Waziri wa Nishati na Madini,Mh. Prof. Sospeter Muhondo pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh. Said Meck Sadick wakati wa uzinduzi rasmi wa Mradi wa Umeme wa Syimbion,uliopo Ubungo jijini Dar.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakichezea mpira maalumu unaojaa nishati kila unapochezwa na nishati hiyo kutumika kuwasha taa ama kuchajia simu wakati wa uzinduzi wa Umeme kwa Afrika kwenye mtambo wa umeme wa Symbion Ubungo jijini Dar es salaam leo.
Rais Jakaya Kikwete na Mgeni wake Rais Barack Obama wa Marekani,wakisikiliza maelezo juu ya mpira unaoweza kufua umeme.
Rais Barack Obama wa Marekani akipiga kichwa mpira huo wenye uwezo wa kufua umeme.
Rais Barack Obama wa Marekani akizindua rasmi mpango wa marekani wa Umeme kwa Afrika kwenye mtambo wa umeme wa Symbion Ubungo jijini Dar es salaam leo.
PICHA NA IKULU
Jamani huwa nikisema mazoezi ni muhimu sana watu wanakuwa hawaeeelewi, Unamuoni Rais Obama alivyo fit? Yaani mzee anadundisha mpira utadhani kijana wa miaka 15!!! Safi sana. Watanzania wenzangu tujitahidi na mazoezi ni muhimu sana kiafya.
ReplyDeleteNi kweli kabisa mdau hupo juu kuhusu mazoezi, michell obama nae yuko fit kishenzi, anapigaga push ups za kufa mtu, nilimuona kwenye show moja ya ellen degeneres alipiga push ups audience wakabaki midomo wazi, na anapinga sana obese children hapa states, hope bongo wataiga mifano na kuipa kipaumbele michezo
ReplyDeletemwandishi wa kwanza na wa pili ni mmoja anajiunga mkono.
ReplyDeletekinda funny ukilazimisha point
Anony wa kwanza na wa pili mmemuona huyo wa wengine tu, wenu hamukuziona hizo dana dana zake! Vipofu wakubwa nyie wa macho na akili, tena watumwa.
ReplyDeleteMichuzi ifikie wakati mtu asipoweka jina lake humu basi asitoe maoni, tumechoka na utumbo.
Yeeeess nimeipenda hyo.chek anavyo piga danadana utadhan mchezaj wa kimataifa bt z not.wengi wakishakua ma famous wanaona kufanya mazoez ni ushamba kumbe waaaaaaaap ni kujenga mwili tena Kwa afya.tanzania tuige mifano ya wenzetu tuache kuabudiana ni ushamba usio na kipimo....yeeeeera ila niliholdiwa sehem wkat naingia mzigon port kisa et ..................,...duuuuuuuuu nlitamn kulia wajameeeeeeen
ReplyDeleteJAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA NI NYUNDO KUBWA!
ReplyDeleteAhhh si mchezo tumefunika!
KENYA:
ReplyDeleteHabari za leo?
Raisi Obama ameodnoka jana na katoa siri ya kuwa yeye ni Mjaluo wa Tarime-Musoma Tanzania na sio Mjaluo wa Kenya, kule Kisumu walihamia tu kwa ajili ya uvuvi wa Kamongo ktk Ziwa Victoria!
Nimempenda Jakaya alivyopoz na mpira, kama Mess.................
ReplyDelete