Timu ya Taifa ya Uganda (The Cranes) inatarajiwa kuwasili nchini kesho (Julai 11 mwaka huu) tayari kwa mechi ya kwanza ya mchujo kusaka tiketi ya Fainali za Afrika kwa Wachezaji wa Ligi ya Ndani (CHAN) dhidi ya Taifa Stars itakayochezwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam. 
The Cranes itatua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 5.30 asubuhi kwa ndege ya Air Uganda ambapo itafikia hoteli ya Sapphire iliyoko maeneo ya Kariakoo. 
Waamuzi wa mechi hiyo ambao wanatoka Burundi nao watawasili kesho saa 9.35 kwa ndege ya Kenya Airways. Naye Kamishna wa mechi hiyo Tesfaye Gebreyesus kutoka Eritrea atatua nchini keshokutwa alfajiri kwa ndege ya EgyptAir. 
Maofisa wote hao wa mechi hiyo watafikia hoteli ya New Africa. Mkutano wa maandalizi ya mechi utafanyika Ijumaa saa 10 jioni Uwanja wa Taifa, na utakuwa chini ya Gebreyesus.

Boniface Wambura
Ofisa Habari
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...