Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Matamba wilayani Makete,wakati wa Ziara yakr Mkoani Njombe.
Sehemu ya wananchi wa kata ya Matamba wilayani Makete,wakimsikiliza Waziri Mkuu (hayupo pichani).

Na Edwin Moshi,Makete.

Serikali imesema itahakikisha hivi karibuni barabara ya Chimala – Matamba itapandishwa hadhi kutoka halmashauri ya wilaya ya Makete na kuwa ya mkoa kwa kuwa halmashauri ya wilaya ya Makete ina mzigo mkubwa wa kuihudumia barabara hiyo ambayo ni msaada mkubwa kwa wanamatamba

Hayo yamesemwa na waziri mkuu Mizengo Pinda wakati akihutubia mkutano wa hadhara uliofanyika katika kata ya Matamba wilayani Makete.

Waziri Pinda amesema amepita kwenye barabara hiyo ambayo ina mlima na kona kali zipatazo 57 na kujionea hali halisi ambapo amesema barabara hiyo inatakiwa kufanyiwa matengenezo makubwa ambapo kwa uwezo wa halmashauri itakuwa na mzigo mkubwa wa kuihudumia barabara hiyo.

“kwa kweli halmashauri ya makete itakuwa inapepesa tu kuihudumia biashara hiyo, inahitaji matengenezo makubwa ikiwemo kuibomoa miamba na milima, hivyo nikirudi wizarani nakwenda kumuandikia barua Magufuli kwa mkono wangu mwenyewe ili aipandishe hadhi iwe ya mkoa, maana mkoa wenu umeshaandika maombi ya barabara hiyo kupandishwa hadhi” alisema waziri mkuu Pinda.

Hatua hiyo pia inafuatia ombi alilolitoa mbunge wa makete ambaye pia ni naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge kumuomba waziri mkuu kusaidia barabara hiyo ipandishwe hadhi kwani itasaidia wakulima wadogo kusafirisha mazao yao kwenda Mbeya na hata kwa usafiri wa kawaida kwani ni fupi.

Katika hatua nyingine waziri mkuu Pinda ametoa sh. Milioni 10 kwa ajili ya kituo cha fema matamba ambacho kinalea watoto yatima ambao hawana wazazi wote wawili.

Kituo hicho ambacho kipo chini ya kanisa kimeonesha kumgusa waziri mkuu Pinda ambapo amesema kama sio kituo hicho hawafahamu watoto hao wangekuwa wapi hivi sasa hivyo kuunga mkono uamuzi uliofanywa na kituo hicho kwa kutoa kiasi hicho cha fedha.

Akiwa matamba waziri mkuu amesomewa taarifa ya wilaya na kuu wa wilaya ya Makete Josephine Matiro.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...