Mkurugenzi Mtendaji wa Makampuni ya ASAS,Salim Abri  akizungumza na wakazi wa mji wa Iringa na vitongoji vyake waliojitokeza kwenye semina ya kamata fursa twenzetu.ASAS amejitolea kiasi cha shilingi milioni tano kwa ajili ya kusaidia vikundi vitakavyoamua kutumia fursa ya kulima vitunguu na kuendelea kuwa wajasiliamali katika fursa mbalimbali. 
 Mdau mkubwa wa michezo nchini Fredrick Mwakalebela naye alipata wasaa wa kuzungumza na wakazi wa Iringa na kutoa kiasi cha shilingi milioni moja kwa ajili ya kuwawezesha wakazi wa mkoa huo watakaoweza kutumia fursa ya rasilimali zilizopo mkoani hapo.
 Mwakilishi kutoka NSSF Makao Makuu Salim Khalfan, akizungumzia Fursa kwa upande wa NSSF wanavyoweza kuitumia wakazi wa Iringa katika kupata mikopo itakayowawezesha kujikwamua kimaisha.
 Mkurugenzi wa vipindi na uzalishaji wa Clouds Media Group, Ruge Mutahaba akihitimisha semina ya Kamata fursa twenzetu mepema leo mchana ndani ya mkoa wa Iringa.
 Baadhi ya wakazi wa Mkoa wa Iringa wakifuatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa kwenye semina ya Fursa kwa vijana iliyofanyika kwenye ukumbi wa Chuo cha Mtakatifu Dominic  mjini Iringa,ambapo watu mbalimbali wamepata fursa ya kujua namna ya kutumia sasilimali zilizopo mkoni humo kwa ajili ya kujikwamua kimaisha.PICHA ZAIDI BOFYA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...