Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Diana Melrose akitoa hotuba fupi kwenye ufunguzi wa Mkutano wa siku moja wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani uliofanyika leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam. Mkutano huo umeandaliwa na Mfuko wa Usalama Barabarani kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani(WHO).
Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja akiwasilisha Mada kuhusu uimarishwaji wa Miundombinu ya Usalama Barabarani katika Mkutano wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani. Kamishna Jenerali wa Magereza alikuwa ni Miongoni mwa Wadau walioalikwa kushiriki katika Mkutano huo wa masuala ya Usalama Barabarani kutokana na Jeshi la Magereza kuwa lipo mbioni kufungua Kiwanda cha kutengeneza Kofia ngumu katika Gereza Kuu Ukonga.
Baadhi ya Washiriki mbalimbali na Wadau wa Masuala ya Usalama Barabarani wakifuatilia kwa makini mada mbalimbali zilizowasilishwa katika Mkutano wa siku moja wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani uliofanyika leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Diana Melrose(wa pili kushoto) akisikiliza mada fupi iliyowasilishwa na Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani Tanzania, DCP. Mohammed Mpinga katika Mkutano wa kujadili masuala ya Usalama Barabarani uliofanyika leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam(wa kwanza kushoto) ni Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja.
Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania akiwa katika picha ya pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Usalama Barabarani wa Kamisheni ya Usalama Duniani, Saul Billingsley(wa kwanza kulia),Kamanda wa Polisi Usalama Barabarani Tanzania, DCP. Mohammed Mpinga(wa pili kulia), Kamishna Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa kwanza kushoto) na Mwenyekiti wa Mkutano huo wa Masuala ya Usalama Barabaran, Kelvin Watkins leo Septemba 2, 2013 katika Hoteli ya Hyatt Regency, Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Kamanda Mpinga umetokelezea, "Usalama barabarani unaanza kwangu, kwako na sisi sote" watanzania tushiriki kikamilifu kutokomeza vifo na majeruhi wanaotokana na ajali za barabarani.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...