Mmoja wa Wasanii mahiri katika anga ya muziki wa kizazi kipya,Ommy Dimpoz akiwaimbisha mashabiki wake usiku huu kwenye uwanja wa Samora,ambapo tamasha la Serengeti fiesta linafanyika usiku huu.
Msanii aliyewahi kuiwakilisha vyema shindano la BSS,Walter Chilambo akiimba jukwaani usiku huu,wakati tamasha la Serengeti Fiesta 2013 likiendelea kwenye uwanja wa Samora.
Mmoja ya wasanii wa kike wanaokuja kwa kasi kwenye anga ya muziki wa Bongofleva,Neylee akiimba kwa hisia jukwaani usiku huu.
Sehemu ya umati wa watu wakifuatilia tamasha la Serengeti Fiesta usiku huu ndani ya uwanja wa Samora.
Mzee wa mahaba kutoka Manzabay,Cassim Mganga akiwaimbisha mashabiki wake jukwaani usiku huu mbele ya maelfu ya wakazi wa Iringa na vitongoji vyake kwenye tamasha la Serengeti Fiesta 2013.PICHA ZAIDI LIVE HAMIA MICHUZIJR.BLOGSPOT.COM







Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...