Viunga vya mji wa Iringa, Mkoa wa Iringa ni Mwenyeji wa Wa Wiki ya Vijana Kitaifa, kumbukumbu ya Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Kilele cha Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2013.
Askari wa Kikosi cha Zimamoto wakitoa elimu kwa baadhi ya wakazi wa Iringa namna kutumia vifaa vya kuzimia moto na jinsi ya kukabiliana na majanga ya moto katika maeneo yao leo wakati wa maonesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa yanayofanyika mkoani Iringa.
Baadhi ya wakazi wa Manispaa ya Iringa waliofika katika banda la maonyesho la VETA Iringa wakipata maelezo ya bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na na VETA kutoka kwa Bi. Oliva Adriano mwanafunzi wa mwaka wa 3 katika chuo cha Ufundi (VETA) mkoa wa Iringa.
Vijana wa Chuo cha Ufundi Stadi (VETA) mkoa wa Iringa wakionyesha ujenzi wa nyumba za gharama nafuu wakati wa Maonyesho ya Wiki ya Vijana Kitaifa mkoani Iringa leo.
Baadhi ya Watoto wakiangalia banda la Vijana kutoka mkoa wa Dar es salaam na bidhaa mbalimbali zilizotengenezwa na Vijana hao leo katika viwanja vya Mlandege mkoani Iringa. Picha na Aron Msigwa -MAELEZO.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...