Na Sultani Kipingo
Ushindi kwa Ujerumani
ulitegemewa, ukizingatia Ureno ni kama
kwamba timu ya mtu mmoja – Ronaldo. Lakini ukweli ni kwamba isingekuwa hivyo
baada ya Pepe kuoneshwa kadi nyekundu katika kipindi cha kwanza. Ila mechi hii
haikuwa ni juu ya Pepe, na wala haikuwa ya Miroslav Klose, na hata haikuwa juu
ya Cristiano Ronaldo. Mechi yote hii ilikuwa juu ya Thomas Muller.
Mshambuliaji huyu wa
Ujerumani tayari ameshaanza mbio kuelekea kwenye mstari wa mwisho wa mfungaji
bora wa michuano, baada ya kupiga mabao matatu (hat trick), na kuendelea
kuinyanyasa Ureno na Ronaldo wao muda wote wa mchezo.
Hakika michuano hii ya
Kombe la Dunia huko Brazil imekuwa ni ya kuvutia hadi sasa. Na mechi ya
Ujerumani na Ureno ilisemwa kuwa mtanange wa mwaka. Na Ilikuwa hivyo kwa
Ujerumani kuondoka na ushindi wa mabao 4-0



Ujerumani wameshinda, Hongera, lakini mimi nawaonea huruma kama hawana haya wanapoona video ya mshambuliaji wao Muller cheating.Football is played by the rules, so if someone is prepared to cheat by acting like a baby so that the opponent is sent off, where is fair play? Pepe ni mpumbavu,hana haki ya kumgusa mchezaji mwingine kwa hasira, lakini Muller alikuwa na nia moja tu, nayo ni kumdanganya refa. FIFA waangalie video na kumnyoa nywele Muller
ReplyDelete