Na Faustine Ruta, Bukoba.

BARAZA la Madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba Mkoani Kagera limewasimamisha kazi Watendaji sita wa Halmashauri kupisha uchunguzi wa upotevu na ubadhirifu wa milioni 851 za mfuko wa barabara, Mfuko wa Afya, na Mfuko wa Jimbo zilizotumika bila kufuata utaratibu na kanuni za wa fedha. 

Watendaji hao sita waliosimamishwa katika kikao cha Baraza la Madiwani cha tarehe 28.01.2016 walihusika na ubadhilifu wa fedha hizo kwa kuzitumia bila kufuata kanuni, taratibu na sheria za kuomba idhini ya kuhamisha vifungu vya fedha au kubadilisha matumizi yake kutoka fungu moja kwenda fungu lingine. 
Hayo yalibainishwa na Kamati ya Wataalamu sita iliyoundwa na Mkuu wa Mkoa Mhe. Mongella katika kikao cha Bodi ya Barabara kilichofanyika tarehe Januari 21 mwaka huu Mkoani Kagera na kuiagiza Kamati hiyo kuchunguza upotevu wa fedha hizo mara baada ya Mhandisi wa Halmashauri hiyo kuwasilisha taarifa ya matengenezo ya barabara na madaraja kwa mwaka wa fedha 2014/2015. 
Kamati hiyo ya wajumbe sita iliyoongozwa na Katibu Tawala Msaidizi Miundombinu Sekretarieti ya Mkoa wa Kagera Bw. Sabora Wambura na ilipewa siku tano iwe imekamilisha taarifa yake.
 Aidha, taarifa ya Kamati hiyo iliwasilishwa mbele ya Mkuu wa Mkoa, Baraza la Madiwani, Watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukoba, Kamati ya Ulinzi na Usalaama ya Mkoa na Wilaya Januari 27 mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...