Chama cha riadha kwa watu wenye ulemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee [TPC) kimejipanga kushiriki katika mbio za Kilimanjaro Marathoni kwa kudhaminiwa na kampuni ya GAPCO Tanzania wikiendi hii.
Akiongea na wanahabari jijini Dar Es Salaam, Katibu Mkuu wa TPC, Peter Sarungi, wakati wa kutoa shukrani zake kwa GAPCO, kampuni inayoongoza katika uuzaji wa mafuta Tanzania kwa kudhamini mashindano ya Mbio za Kilimanjaro Marathoni za KM10 kwa watu wenye ulemavu.
Alieleza kwamba mashindano ya mbio za Kilimanjaro marathon za 10KM kwa walemavu ambazo zinadhaminiwa na GAPCO ni shindano linalojumuisha baiskeli za walemavu zenye matairi matatu zenye viwango vya kimataifa. Shinando litafanyika tarehe 28 Februari 2016 sambamba na mbio za Kilimanjaro Marathon Moshi, Kilimanjaro na usajili utaanza tarehe 26 Februari 2016. “Mbio hizi ni kwa ajili ya walemavu wote wa Kitanzania, ambapo 60 kati yao watakuwa wakidhaminiwa na GAPCO kushiriki kutoka Dar Es Salaam, Arusha, Moshi na Zanzibar” aliongeza.
Tangu GAPCO ilipoanza kudhamini Marathon mwaka 2011, wameshuhudia maendeleo chanya mwaka hadi mwaka katika ubora wa mashindano. “ Tunashukurum jitihada za GAPCO, si tu katika kufanikisha shindano hili kupitia udhamini wake lakini zaidi ni kutoa msaada wa mahitaji maalumu kwa washiriki wenye ulemavu katika mfumo wa chakula na usafiri.” alisema MrSarungi. “Pia tunafuraha kuhusu kuongezeka kwa zawadi ya fedha taslimu kwa mshindi ambapo ni Tsh. 1,000,000 kiasi hiki kinaweza kubadili maisha ya washindi.
Sarungi amewasihi watanzania kujitokeza kwa wingi kuwashangilia wanariadha watakaoshiriki mbio hizi. “Tunataraji kushiriki na tunachukua nafasi hii kuwakaribisha Watanzania kujitokeza na kuwapashangilia wanariadha wetu katika tukio hili”.
Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (Tanzania Paralympic Committee [TPC]) ni chama cha kitaifa na kimataifa kinachotambulika na Serikali kupitia Baraza la Sanaa Tanzania na Chama cha ridhaa kwa walemavu cha Kimataifa (International Paralympics Committee [IPC]). TPC imekusudia kuwaleta pamoja wanariadha walemavu kutoka Tanzania kupitia matawi ya kimikoa na kiwilaya na makundi mengine yenye hulka zinazoshabihiana (shule za walemavu na timu za michezo).
Katibu Mkuu wa Chama cha riadha kwa walemavu Tanzania (TPC), Peter Sarungi akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam leo, wakati akitoa shukrani zake kwa kampuni ya uuzaji wa mafuta nchini ya GAPCO, kwa kuwadhamini kwenye mashindano ya Mbio za KM10, za Kilimanjaro Marathoni kwa watu wenye Ulemavu, Linalotarajiwa kufanyika tarehe 28 Februari 2016, Mkoani Kilimanjaro.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...