Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) imetoa ripoti ya robo mwaka tangu ianze kufanya uchunguzi wa Virusi vya Homa ya Ini ( Hepatitis B) na kutoa tiba ya ugonjwa huo kwa kutumia dawa ya Tenofovir .

Akitoa taathimini hiyo leo jijini Dar es salaam,  Daktari Bingwa wa Magonjwa ya Ini na Matumbo John Rwegasha amesema  muamko ni mkubwa  ambapo katika kipindi cha robo mwaka , Hospitali ya Taifa Muhimbili imesajili wagonjwa  950 .

Akifanunua amesema  hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu idadi  ya wagonjwa itaongezeka na kufika   1800  .Hata hivyo kati ya hao , wagonjwa 540 ndio wamerudi tena Hospitalini kwa ajili ya kuendelea na mchakato wa uchunguzi huku wagonjwa wengine wakishindwa kufika kutokana na sababu za mbalimbali hususani za kiuchumi , nakuongeza kwamba waliopo kwenye tiba ni  wagonjwa 40.

‘’Idadi ya wagonjwa imeongezeka mara dufu hadi kufikia mwishoni mwa mwaka huu watafika wagonjwa 1800  lakini pamoja na changamoto hiyo hatuwezi kusimamisha huduma tutaendelea kutoa huduma kwani kwa upande wa dawa tumejidhatiti kwa miaka mitano , wagonjwa  hawa wanatakiwa wafanyiwe uchunguzi  ili aanze kutumia dawa lakini  si wote wanaohitaji dawa’’ amesema DK. Rwegasha.
  Mkurugenzi wa Huduma za Tiba katika hospitali hiyo, Dk. Hedwiga Swai akisisitiza watu kujitokeza kupima afya ili kuthibiti homa ya ini pamoja na magonjwa mengine.

 Daktari Bingwa wa Magomjwa ya Mfumo wa Chakula na Ini, John Rwegasha wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) akizungumza katika kongamano jinsi ya kudhibiti na kutibu magonjwa ya mfumo wa chakula na ini.
 Baadhi ya watumishi wa hospitali hiyo wakiwamo madaktari na wauguzi wakifuatilia kongamano hilo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...