Na Avila Kakingo,Globu ya Jamii.

ASASI ya kiraia ya Tushikamane pamoja  foundation imeiomba serikali kuwapa kibali cha kuwaruhusu kuanza kuwatunza wazee katika nyumba ya asasi hiyo iliyopo Kwembe Manispaa ya Ubungo jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza wakati wa kuadhimisha siku ya wazee duniani, Mwanzilishi wa asasi ya kiraia ya Tushikamane pamoja, Rose Mwapachu  amesema kuwa kwa sasa wameshatuma  maombi ya kupata kibali kwaajili ya wazee kukaa katika nyumba waliyoijenga.

"Kwa sasa tumeshatuma maombi serikalini ya kuomba kibali kwaajili ya wazee wasio na ndugu na wasiojiweza kukaa katika nyuma hii tuliyoiandaa kwaajili ya wazee hawa."

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa kusheherekea siku ya wazee, Rose Mwapachu amesema kuwa nyumba hiyo ni kwaajili ya wazee wasiokuwa na ndugu na wasio na sehemu za kuishi ndio watakao kuja kuishi hapa. "Hivyo kwa wazee na wasio na ndugu wala watoto ndio wataishi katika nyumba hii ili kuepusha watu wa madai au kuja kudai mirathi hapa." Amesema Rose Mwapachu.

Kwa upande wa serikali mwakilishi wa  Mkurugenzi wa manispaa ya Ubungo,  Zainabu Mwafilamba amesema kuwa Maombi ya Tushikamane pamoja Foundation tumeyaona na yanafanyiwa kazi.Na kwa upande wa wazee wasio na makazi na wasio na ndugu jijini Dar es salaam wamewashukuru Tushikamane Pamoja Foundation kwa kuwajali kama wazazi wao.

"Sisi wazee wa Dar es Salam tunawashukuru sana Tushikamane pamoja foundation kwa kutujali sisi wazee Mungua awajalie kila lenye heri watu wote wanaowajali wazee kama sisi".Pia wamesema kuwa pale tulikuwa na upweke sasa tunajiona kama watuwalio na ndugu kwa mchango wa Tushikamane Pamoja  Foundation wanavyojitoa kwetu.

 Tushikamane pamoja Foundation wamungana pamoja na wazee wasio na makazi jijini Dar es Salaam katika kusheherekea siku ya wazee duniani ambayo  hufanyika duniani kote ifikapo Oktoba 1 kila mwaka.
 Baadhi ya wazee wakielekea katika nyumba ambayo imejengwa na wana tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya kulea wazee wasio na ndugu wala watoto jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wazee wakielekea katika nyumba ambayo imejengwa na wana tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya kulea wazee wasio na ndugu wala watoto jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi wa Tushikamane pamoja Foundationi, Rose Mwapachu akizungumza na wazee wakati wa kusheherekea siku ya wazee duniani walipokusanyika leo  katika nyumba iliyojengwa na Tushikamane pamoja Foundation kwaajili ya wazee.
Baadhi ya wageni waliohudhulia siku ya wazee duniani iliyoandaliwa na Tushukamane pamoja Foundation jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wazee.
Baadhi ya wazee wakiwa ndani ya chumba mojawapo katika nyumba ya kulelea waze ya kwembe  manispaa ya ubungo jijini Dar es Salaam.

KWA PICHA ZAIDI BOFYA HAPA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...