Lucas Muyovela na Woinde Shizza Michuzi Tv, Arusha

MWALIMU wa Shule ya Msingi Naan iliopo katika Kata ya Engserosambu tarafa ya Loliondo wilayani Ngorongoro mkoani Arusha Solomon Letato Kipuker(30)anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za kukutwa na silaha ya kivita aina ya AK47 ikiwa na risasi tano zikiwa kwenye magazine.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Juni 4,mwaka 2019, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Johnathan Shanna amesema kuwa tukio hilo limefanikiwa baada ya jeshi hilo kwa kushirikiana na kikosi kazi kabambe na jasiri dhidi ya ujangili na uhalifu wa silaha za moto Kanda ya Ziwa chini ya uwezeshwaji wa tanapa na kufafanua kuwa mtuhumiwa huyo alikamatwa mapema Juni 2 mwaka huu katika Kata Engserosamb.

Amesema mtuhumiwa huyo pia ni miongoni mwa wafanyabiashara haramu wa uingizaji wa silaha za moto ndani ya nchi pia mtuhumiwa huyo anahusishwa na ufanyaji biashara ya nyara za Serikali hasa hasa meno ya tembo pamoja na pembe za faru pia anatuhumiwa kujihusisha na shughuli za ujangili kwa ujumla.

"Mara baada ya kumuhoji alikiri kumiliki silaha hiyo ya kivita kwakushirikiana na watuhumiwa wengine ambao bado wanatafutwa aidha baada ya kumuhoji alisema silaha hizo pia amekuwa akizikodisha katika mapigano ya kikabila baina ya jamii za wasonjo, watemi pamoja na wamasai pia wamekuwa wakitumia katika matukio ya ujambazi na utekaji wa Wawatalii na wananchi na mali zao,"amesema Shanna.
Wakati huo huo Jeshi la Polisi limefanikiwa kukamata silaha Aina AK47ikiwa na risasi moja iliyokuwa imetekelezwa kwenye ofisi ya Kijiji cha Mbukeni Kata, Liliondo baada ya jeshi hilo kupata taarifa zakiitelenjensia kubaini uwepo wa bunduki.

Kamanda huyo amesema katika tukio lingine jeshi la polisi linawashikilia majangili sugu wakiwa na nyara za Serikali tangu Juni 30 mwaka huu katika kitongoji cha Maji ya Chai wilayani Arumeru.

Amesema jumla ya watuhumiwa watatu ambao majina yamehifadhiwa wameojiwa na wamekiri kujihusisha na biashara ya ujangili wakiwa na vipande vinne vya meno ya tembo walivyokuwa wamehifahi kwenye mifuko ya sandarusi.
Kamanda amesema watuhumiwa wote watafikishwa Mahakamani pindi upelelezi utakapo kamilika.Ametoa mwito kwa wananchi kuendelea kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa sahihi zitakazo wezesha kuimarisha usalama wa raia na mali Zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...