Uongozi wa Chuo kikuu cha Sokoine cha kilimo SUA umewafuturisha wanajumuia wa kiislamu wa SUA chuoni hapo.
Lengo la futari hiyo ni kuwakutanisha pamoja Wafanyakazi na wanafunzi chuoni hapo ili kubadilishana mawazo,kufahamiana na kujenga mahusiano bora miongoni mwao.
Hafla hiyo ilijumuisha viongozi mbalimbali wa BAKWATA Mkoa ambao walipata nafasi ya kuzungumza na kuelezea maana nzima ya Funga na umuhimu wa elimu kwa Waislamu.
Mwenyekiti wa Jumuiya wa Waislamu SUA Anaitwa Profesa Wahab Kimaro akitoa neno katika wanajumuiya namna alivyoagiza Mtume Mohammad kuhusiana na Mwezi Mtukufu wa Ramadhan
Imam wa Msikiti wa SUA, Said Msuya akitoa mawaidha wakati wa Futari iliyoandaliwa na Chuo Kikuu Cha Kilimo cha Sokoine kwa ajili ya wanajumuiya wa wakiislaam wa Chuo hicho.
Makamu wa Mkuu wa Chuo Profesa Raphael Chibunda(Mwenye Kanzu Nyeupe katikati Mbele) Akifurahia jambo na Viongozi wa BAKWATA mkoa wakati viongozi mbalimbali wakitoa salamu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...