Mwanafunzi wa shule ya Sekondari Mlangai akinawa maji tririka yaliyowekwa nje ya darasa kabla ya kuingia ndani.
Wanafunzi wa shule ya sekondari
Mlangai wakiwa wamekaa kwa kuzingatia vigezo vya umbali wa mita moja
kama walivyopangwa na walimu wao.
Wanafunzi wa shule ya sekondari Bungu wakiwa wanatoka darasani wakati wa Mapumziko.

Madarasa ya shule ya Sekondari Mlangai yakiwa yamewekewa vifaa vya kunawia maji tiririka.
…………………………………………………………………………
Na Mwandishi Wetu, Korogwe
Ikiwa ni wiki Chache
Tangu kufunguliwa kwa shule za Msingi na Sekondari nchi nzima mara baada
ya kufungwa kutokana na tishio la homa kali ya mapafu inayosababishwa
na Virusi vya Covid 19 Shule za Sekondari Korogwe zimejipanga kuchukua
tahadhari dhidi ya ugonjwa huo.
Mwandishi wetu
amepata kutembelea baadhi ya shule za sekondari zilizopo pembezoni mwa
Wilaya hiyo za Bungu na Mlangai na kukuta utaratibu wa kunawa mikono na
vipeperushi umezingatiwa huku Changamoto ikiwa ni kwenye uvaaji wa
barakoa kwa wanafunzi.
Degratius Mapima ni
Mwalimu Mkuu wa shule ya Sekondari Mlangai hapa anaeleza namna
walivyoweza kuandaa vifaa na mazingira ya kujisafisha kabla ya kuingia
darasani.
“Tuliwapa elimu siku
ya kwanza tu walivyoingia shuleni jinsi ya kujikinga, ikiwa kunawa
mikono kila wakati na matumizi sahii ya barakoa” anasema mapima.
Anasema kama shule wameweza kuweka vifaa vya kunawia kila mlango wa darasa na eneo la geti la kuingilia shuleni.
Kwa upande wake
Mwalimu mkuu wa shule ya Sekondari ya Bungu, Mohamed Mkono ametaja kuwa
licha ya kuweka tahadhari zote lakini bado kunachangamoto ya wanafunzi
kutovaaa barakoa .
“Licha ya tahadhari
tulizoziweka bado tunachangamoto ya Wanafunzi wengi hapa awavai barakoa
licha ya kuwaambia pia tatizo la social distance bado ni tatizo kwa
vijana wetu kama unavyojua watoto wetu wanapenda michezo ya kukaribiana
ndio maana hata kwenye kazi za makundi unawakuta wapo karibukaribu hivyo
aiepukiki” anasema Mwalimu Mkono.
Anamaliza kwa kusema
kuwa kicha ya changamoto ya kukaa nyumbani kwa takribani miezi mitatu
wanafunzi walirudi shule wakiwa na hamasa kubwa mno tofauti na mika ya
nyuma ambapo shule zikifunguliwa ukuta wanafunzi wanachwlewa.



Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...