NDG. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI, MWENYEKITI WA CCM NA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KUCHUKUA FOMU ZA KUGOMBEA URAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO KWA TIKETI YA CCM
_______________

Makao Makuu ya CCM, Dodoma
05 Agosti 2020

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinapenda kuujulisha umma wa wana CCM na watanzania kwamba Ndg. John Pombe Joseph Magufuli Mwenyekiti wa CCM, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mgombea wa nafasi ya Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kesho tarehe 06 Agosti, 2020 atachukua fomu ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM katika Ofisi za Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi Tanzania (NEC) zilizopo Njedengwa Jijini Dodoma.

Ndg. Magufuli atachukua fomu majira ya saa 3:00 asubuhi na atasindikizwa na watu wachache wakiwemo viongozi wakuu wa chama, ikiwa ni kutekeleza matakwa na maelekezo ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC).

Ndg. Magufuli ambaye ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania anachukua fomu hiyo ili kugombea Urais kwa kipindi cha pili katika Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika tarehe 28 Oktoba, 2020.

Baada ya kuchukua fomu, Ndg. Magufuli atakwenda katika Ofisi za Makao Makuu ya CCM Jijini Dodoma (White House) ambako atakutana na wanachama, wapenzi na wakereketwa wa CCM na kuwasalimu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...