ASEMA SERIKALI IMEJIPANGA KUKABILIANA NA ATHARI ZITAKAZOWEZA KUJITOKEZA.

Kufuatia tahadhari iliyotolewa na Mamlaka ya Hali ya hewa Tanzania TMA dhidi ya kimbunga "Jobo", Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Aboubakar Kunenge amesema tayari Ofisi yake, Halmashauri zote tano za Mkoa kwa kushirikiana na Vyombo vya ulinzi na usalama vimefanya maandalizi yote muhimu kuhakikisha usalama wa Wananchi unazingatiwa.

Akizungumza na Vyombo vya Habari leo, RC Kunenge amesema Vikosi mbalimbali ikiwemo Jeshi la Polisi,Zimamoto na uokoaji, Tanzania Red Cross, Taasisi za huduma za Afya, magari ya Wagonjwa, waratibu wa maafa wamejipanga kukabiliana na athari zitakazoweza kujitokeza.

Aidha RC Kunenge ametoa wito kwa wananchi wa Mkoa huo kuhakikisha wanachukuwa tahadhari ikiwemo kufuatilia taarifa Za TMA, watumiaji wa vyombo vya Majini Katika Bahari ya Hindi kuchukuwa tahadhari huku akisema ni vyema watu wakatulia majumbani wakati mvua inaponyesha na kuepuka kupita kwenye mikondo ya Maji yanayotembea.

Hata hivyo RC Kunenge amesema taarifa zilizotolewa na TMA zinaonyesha mgandamizo wa hewa umepungua Nguvu Katika usiku wa kuamkia leo Aprili  24 na kufanya kimbunga kuwa hafifu lakini bado kinaendelea kusogea sogea maeneo ya Pwani na hadi kufikia usiku wa kuamkia leo Jumamosi kimbunga kipo Takriban Kilomita 200 kutoka Pwani ya kisiwa Cha Mafia.

Pamoja na hayo amesema kwa Sasa athari zinazoweza kujitokeza katika Mkoa huo ni Mvua nyingi Katika baadhi ya maeneo, upepo mkali na Mawimbi Makali.


 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...